TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Kuna baadi ya vyama vimeanza kuchakachua zoezi la kupiga kura mapema sana kabla hata tarehe za uchguzi mkuu wa mwaka huu kuakaribia.
Taarifa tulizopata toka huko Mkoani mbeya wilayani Kyela ni kwamba katika kata ya Itunge kitongoji cha Mwandekesye wilayani Kyela, balozi wa kitongoji Boniface ameonekana akipita kila nyumba na kuomba kitambulisho cha mpiga kura na anachokifanya ni kuandika namba za kitambulisho na mwaka aliozaliwa mwenye kitambulisho.
Habari hii imetolewa na Radio Kyela FM katika kipindi chake cha,  kumekucha na Kyela Fm.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Meneja wa redio hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook ambaye alisema alizungumza na wananchi zaidi ya sita ikiwa ni baadhi tu ya wale walioombwa kitambulisho wakathibitisha kuwepo kwa jambo hilo.
Pia limfuata mtuhumiwa na kutaka maelezo kwake kwa ufupi amekiri na kusema ni agizo kutoka uongozi wa juu na wameagizwa mabalozi kufanya zoezi hilo.
Afisa uchaguzi wilaya ya Kyela Omary Mungi baada ya kumpa taarifa amesema ni kinyume cha sheria hivyo ameahid kulishughulikia mara moja.


Source Kyela FM

0 comments :

 
Top