TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Zitto Kabwe, kupitia ukurasa wake wa facebook alikanusha kuhusu yeye kuzomewa Tunduma Mkoani Mbeya kwa kuitwa Yuda, yaani maana yake ni msaliti. ufuatao ni ujumbe ambao alikuwa ameandika na ukanukuliwa na ukurasa wa facebook wa EATV.
"Kuna watu wanasambaza video kuwa eti nimezomewa Tunduma. Sijawahi kufanya mkutano wowote wa kisiasa Mjini Tunduma. Ni wanasiasa uchwara tu ndio wanaweza kujitekenya na kucheka wenyewe. Mwenye picha au video yenye kunionyesha dhahiri kuwa nilikuwa Tunduma aweke hadharani. Siasa za kuzusha uongo hazitaivusha nchi hii. Waliotumwa kufanya kazi hiyo wanawadanganya waliowatuma. Sisi tunaendelea kufyeka mapori"
Lakini sisi tunakuletea ushahidi unaothibitisha ukweli wa mambo jinsi ulivyokuwa.

0 comments :

 
Top