TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749




Nani atasema 2018 Tanzania itakuwepo Kombe la Dunia  pale Mwanza,Dares Salaam, au Arusha ya Russia? Tutamwita chizi, tena chizi aiyejitambua .Kuna mwanafalsafa mmoja anaitwa Winston Churchill aliwahi kusema “Success is not final,failure z not fatal: It’s a courage to continue that count”.
'Courage' yakusonga inapatikana wapi?   kama 'failure' ni  za kutengeneza na sio changamoto za kikazi tu.

Mtu akisema hakuna changamoto  huo ni  'upuuzi' nikimaanisha upuuziaji wa mambo,ila makosa tengenezi kama una fikra pana huwezi kubaliTaifa Stars itachukua Kombe la Mataifa ya Afrika miaka mitatu mbele.Unakataa tu hakuna namna,ukubalije, hata miujiza sio kirahisi hivyo.

Tutashangaa Yanga  kuchukua klabu Bingwa Afrika mwakani kama wakishinda ligi. Ni kuwa haiwezekani. Kwenye 'imani' bila ubidii ni kazi bure vitabu vya dini vimeandika. Wakristo  wenzangu wanaamini katika mstari usemao “Asiyefanya kazi na asile”. Uwekezaji,Uongozi mbovu, Makocha pangiwa kikosi,Viwanja vibovu, na Mashabiki kukwepa viingilio viwanjani, hapo hujafanya kazi,unata kaule(mafanikio na vikombe) nani kasema? Mganga wa Msata.

Ratiba za ovyo, Bodi ya Ligi ilichemsha, hasa msimu uliopita 2014/15 ratiba ilibadilika pasipo uchunguzi tosha kwa mwelekeo wa ligi za ndani na nje. Zaidi pale ilipobadilika mara mbili kwa wiki moja pekee, haikuleta mantiki kwa wadau na klabu husika kwa gharama na uungwana kutumika, Prisons ya Jiji la Mbeya ilifika Dares Salaam kwaajili ya mechi yao naAzam, na Bodi ya Ligi kuwataka warudi Jiji Mbeya  wacheze na Yanga baada ya hapo ndipo  warudi Dares Salaam kuvaana na  Azam. Azam na Yanga pia walihitajika kwa mechi za kimataifa, kucheza mechi ndani ya siku nne.Mechi za Ligi na Kimataifa, nini kilitokea.Walifungwa. 
Ratiba ngumu, kupanga.Je mikakati itafanikiwaje Kimataifa zaidi? labda ratiba ya mwaka huu iliyotangazwa juzi italeta jipya kutakuwa na kilichoboreshwa, natamani nione kuna mazuri yenye tija!
Kuna lile  la vyanzo vya mapato ilikuchangia mfuko wa timu ya Taifa ya siku za usoni yaani kuwakata klabu kwa kuchukua  5% za udhamini  na kwa kila tiketi inayouzwa kukatwa shilingi elfu moja.Ushauri wa wadau uliwataka  TFF watafute vyanzo vingine. Hivi TFF imekosa mbinu ya 'kuuzamaneno' kwa Wadau kibao,Mashirika, Taasisi naSerikali  kuwekeza kwa kiasi kikubwa?Mpira kwasasa ni nembo ya biashara kubwa yoyote, hivyo unalipa. 
Hivi viwanja madimbwi, mitaro 'upuuziaji'' usio na tafakuri  nani mmiliki? Jiji(Serikali), Chama, na Watu Binafsi wanahusikaje wasiikwepe aibu endelevu. Pale uwanja wa Kambarage, Shinyanga vyumba vya kubadilishia nguo havina hadhi  inayotakiwa si Simba, Ruvu Shooting na Mbeya City walilalamika. Kule Sheikh Amri Abeid, Arusha kubwa lilikuwa vyoo vibovu. Michezo pia ni siasa,siasa zisizo na maboresho zinaboa. Sikuwa 'nawashupalia' CCM ila nao ni wanamilikiwaViwanja kadhaa, mfano tosha wao wanavyo vingi kiuwiano. Kambarage-Shinyanga, Jamhuri-Morogoro, SheikhAmriAbeid-Arusha, Mkwakwani-Tanga, vyote hakuna kilichokuwa na afadhali. Arusha na Shinyanga walitangaza kukarabati, sasa je vitaleta hadhi hata ya kitaifa kwani kimataifa ni mbali.Michezo ya Kimataifa utaionea wapi? Kila Siku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, na je ukifungwa kwa ukarabati na sisit tuingoje burudani, yule  Aboubakar Salim "Sure boy" wa Azam nani atamwona na 'michejo' yake. Shambani Uwanja tutalimaje kama ni 'magumashi'. Mwaka huu naamini viwanja  vitaleta burudani alafu kuna Azam  HD mambo yatakuwa “live” tutashudia kwa macho ya ziada, tutaambiana!
Nani anaikumbuka “Taifa Cup” ilileta chachu fulani kuchangamsha ligi kuu, unamkumbuka  Gaudence Mwaikimba akiwa na Mapinduzi Stars(Mbeya), aliibuka mfungaji bora katika michuano hiyo mwaka 2011. Hivi hiyo michuano iko wapi sasa hivi? inaleta vipaji visivyojulikana kwenye ligi kuongeza mvuto. Nimepata faraja na Federation Cup kuwepo kwenye ratiba ya ligi kuu  iliyotoka juzi, safi sana!
Mpira wa kileo ni biashara nani akubali kwenye suala la kujitoa na nguvu anakutana na 'pesaudafu' ,posho za kusubiri miezi kadhaa na heshima za msimu kama kwa Juma Kaseja kwa 'vigelegele' toka Misri 2003 leo wanamwambia  “kauza timu” kwa magoli ya siku moja, yule Peter Schiemiel miaka yote Manchester United hakuwahi kufungwa kizembe? Alifungwa si mara moja.Mbona alidumu. Wazungu wanajua “changamoto za kazi”mtu hana ukamilifu tunajitahidi.Inachukiza kutaja mfano kutoka kwa ‘Wazungu” ilat utafanyaje ,ndio “reality” wapo hatua kadhaa mbele yetu.Usipokubaliana na ukweli, ni ujinga.
Safi mbeya city mmemuelewa JK(Juma Kaseja) kwa mkataba wa miezi sita, sio mbaya!
Klabu kubwa Afrika kama vile  Etoile du Saleh,Al Ahly na Esperance wanalipa wachezaji kuanzia dola 10,000 kwa mwezi, African Lyon  na Coastal Union watatoa kweli na udhamini huu wa Mashirika kutoka Mkoa wa Kilimanjaro(ubahili),wachezaji nao wanajithaminisha kweli au ni Elimu ndogo juu ya maslahi na huduma wanayoitoa klabuni? Bora liende tu au ni 'kuuza sura' pale Azam au Simba na “umaarufu kuonekana” wakipita Posta naMbagala mashabiki tuwaombe kupiga “selfie”.
Athuman Machuppa JKT Ruvu walimchukua  mwaka 1997 kwa uhamisho wa 15,000, enzi hizo ilikuwa na thamani,mchezo haukuwa na kipaumbele kama sasa,haukuwa na nguvu ya kushawishi 'wazazi' ni ajira, msitupeleke kule.
Mapenzi na klabu yapo,ila sikia si kikubwa kama enzi za Mecky Mexime pale Mtibwa Sugar. Mchezaji jua thamani yako utapiga fedha kama Emmanuel Okwi,Yangana Simba wanamjua huyu jamaa vyema misimu miwili iliyopita ,jitambue mchezaji.
Mapenzi na 'Taifa Stars' ni “ automatically”  nani ayatengeneze,tatizo mfumo wa kuweka sawa kuleta faraja kwa Watanzania haujafikiwa. Ari na nia ya kuunganisha Watanzania kwa michezo ulifanikiwa. Enzi za Marcio Maximo tulifanikiwa,usipomshukuru huyu  mbrazili  kwa historia ya hivi karibuni ya Taifa Stars tutakuita “asiyejielewa”.  Uzalendo ulipachikwa kama vile upo kambini Mafinga-JKT  ukiwa  “kuruta”.Unajua nini maana yaTaifaStars. ndo tunalitaka hilo kwa sasa!
Hili la kikosi cha vijana kuanzia miaka 13 na baadaye kujumuishwa chini ya miaka 17, hongera TFF chini ya Rais wake Jamal Malinzi . "Mdogo mdogo" tutafika!
Unamkumbuka kocha Kim Paulsen toka timu ya vijana “Serengeti Boys” mpaka Taifa Stars. Kipindi kile alitisha kwa kiasi chake akiwa Taifa Stars unajua kwanini?Alitokana “makinda” yake kuja kikosi kikubwa. Hichi ndicho kinachotakiwa!

Enzi naanza kuusikia mpira kwa uzuri nilivutiwa na Juma Kaseja na yule marehemu Cristopher Alex “Massawe” ilikuwa mwaka 2003, ilikuwa mechi ya Kimataifa, Klabu Bingwa Afrika Simba dhidi ya Zamalek. Kisa maajabu yao wamenivutia mpaka leo, uliyaona “mapenalti” ya wale Waarabu yalivyomwogopa Kaseja?  Je uliuona mkwaju wa mwisho wa Alex (Christopher)?shujaa wangu huyu ,nakuombea Mwenyezi Mungu akupe heri huko ulipo.
 Leo teknolojia imekua kila kona, na mpira wa Ulaya umetawala dunia, yule Lionel Messi anajulikana kuliko Simon Msuva, huku mtaani wanasema mbio za Gareth Bale yule Mrisho Ngassa hafiki hata robo,Misingi gani inahusika kuanzia ngazi ya chini,ili “dogo”fulani pale Mbagala, Usangi, na Nyamagana  aujue uzalendo.Cha kushangaza kwa sasa anajua jezi nambari 7 aliwah ikuivaa David Beckham,timu ya Taifa na baadhi ya klabu zake alizopitia, lakini  hajui Boniface Pawassa yule aliyekuwa zamani Simba  alivaa nambari ngapi  mgongoni?
Siku hizi uzungu mwingi.Nani anajali? “Mdingi“ wake kakazania mpira wa bongo hauna mvuto,unahisi nini kitatokea kwa “dogo” yule? “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”.
Pale Uwanja wa Taifa, panajaa mahasimu wa Jiji wakichuana, yule wa Msimbazi na Jangwani wakati kule Uingereza haijalishi nani anacheza. Mashabiki watajaza uwanja tu,  lakini  labda kesho Jumamosi kisa “Ngao ya  Jamii” Yanga na Azam patamwagika  sio ,”dogo”  huyu atajua Tanzania kuna Simba naYanga,kama “mdingi” wake anavyowaza. Unajua kitakachotokea kama mambo yasipobadilika?

Ni rahisi kama ilivyo kawaida 'dogo' huyu aliyezaliwa enzi za Rais Jakaya Kikwete yupo madarakani kumjua Christiano Ronaldo kuliko  yule beki mpambanaji wa Azam  Aggrey Morris . Ikowazi. unabisha?


Kwakuwa shujaa wao(starring/hero) alishauawa “scene” ya kwanza.



 PETER C. MMBAGA.

 +255 656 859 045.

0 comments :

 
Top