Na Mayunga Jackson
Nikiwa wiki zima toka nifike shinyanga
Mjini na kutembea wilaya za karibu kama vile Kishapu mkoani Shinyanga
mengi nimejionea, kikubwa ni kiu ya watanzania wa mkoa wa shinyanga
kuchoshwa na CCM.
Nikianza na Shinyanga mjini nimeshuhudia mgombea wa
CHADEMA Ndg Katambi, anaungwa mkono na wananchi wa tabaka lote na rika
lote hapa shinyanga mjini nikiwa maeneo ya Ngokoro na Bugweto,
nilishuhudia watu wakisema mgombea wa CCM Ndg Masele, watu wanadai hata uchaguzi uliopita mwaka 2010 zengwe
lilitawala katika ushindi wake, hivyo mwaka huu kweupee, wana wa Shinyanga
watatumia vichinjio vyao watamkata.
Pengine CHADEMA ina cha kujivunia
kutokana na mchango mkubwa wa marehemu Bob Nyanga Makani, kwa
kukifanya chama hiki kupendwa na maelfu ya watu hapa shinyanga
mjini. Hivyo ninakila sababu ya kuamini mwenyekiti wa BAVICHA Ndg Katambi,
ataibuka kidedea kwa Masele
Kwa upande wa Kishapu
wilaya anayotokea mbunge anayemaliza mda wake wa CCM Ndg Sueleman Nchambi,
hali ya maisha bado inatisha sana nimetembelea kata nne kati ya
ishirini, tatizo kubwa ni maji, wananchi hawana hata visima vya kata. Maji ni shida, wanachimba maeneo na wanatumia maji na mifugo, huduma
ya afya ni mbaya kupindukia nimetembelea kata ya Itilima,
Talaga, Bunambiyu na Ukenyenge, kiukweli, Suleman Nchambi, hajawatendea
haki wana kishapu. Pengine nikipata bahati ya kuonana nae ntapaza sauti
kwa niaba ya wana Kishapu nimuulize fedha za mfuko wa maendeleo ya jimbo
amezitumia kwa mradi gani?? na kipi akiwa kama mbunge anayemaliza mda
wake angejivunia kwa kata tajwa hapo juu.
Nnachokiona kwa sasa nguvu kidogo tu inahitajika kumwongezea nguvu
Mgombea ubunge Chasema, Ndg Mpendazoe, awafikie wananchi wengi wa kishapu
huku akiahidi kutatua kero za maji basi Sueleman Nchambi
kweupee.
Lowasa ameamsha hisia za watanzania waliochoshwa na
utawala wa chama cha mapinduzi hivyo kila sehemu wapo tayari.
Wito
wangu kwa vijana wezangu wenye nia ya dhati na maendeleo ya taifa
letu, tutembee tuende vijijini tutazame matatizo ya watanzania ndo tuje
tujikaze na aibu yetu huku tukisema CCM oyeeee. Vinginevyo huu usaliti
tunaoufanya ni dhambi kubwa mbele ya mungu.
CCM Ilipotufikisha bhaasi
jamani tutoeni fursa kwa UKAWA. Viva Mabadilikoooooooooooo
Lowassaaaaaaaaaa.
0 comments :
Post a Comment