
CCM wanaendelea kujiandalia njia ya kuelekea katika kaburi la Kisiasa
na wamepita njia ile ile ambayo alipita Marehemu PDP(Peoples Democratic
Party) Cha Nigeria.
Chama cha PDP kilipokua kikipambana na Muungano wa UPinzani kupitia
chama cha APC cha Mohammed Buhari nchini Nigeria walijikuta wakikosa
ajenda ya kushawishi wananchi badala yake wakaamua kuwa waumini wa Siasa
za mitaroni kama kupanga matukio ya kuupaka matope upinzani,Kumtakia
Kifo mgombea wa PDP n.k
Nguvu,Akili na Raslimali nyingi walizielekeza huko na matokeo yake
walishindwa uchaguzi kisha baadae wakaanza kulaumiana na kujaribu
kuvunja kamati kuu yao
Kwa Mbinu ileile CCM wamepanga mikakati inayofanana na ya PDP kwa matukio ya wiki
Hebu tazama mikakati yao ya ajabu ajabu
-Wiki ya Kwanza Lowassa alipohamia CHADEMA wao waliwekeza kwenye Tukio la Prof.Lipumba kujiuzulu
-Wiki ya Pili ambayo ilikua wiki ya Kwanza kwa Kampeni Tukio la
Dr.Slaa kwao walilichukulia kama Mtaji kisha wakaendelea kupanga maana
walinogewa.Ndipo walipoanza kupanga na kuelekeza smearing campaign yao
kwa matukio kadhaa in series
-Wiki ya Tatu yaani wiki ya Pili ya Kampeni wakaibuka na siasa chafu
za Udini huku Msemaji wa Chama akiwa kinara kabisa bila aibu kupotosha
na kufanya siasa chafu za Udini ili kupandikiza chuki za kisiasa baina
ya Ukristu/Ulutheri na Dini nyingine
-Wiki ya Nne(Wiki ya Tatu ya Kampeni) Wakaibuliwa watu wawili (Moses
na Letcia) NCCR-Mageuzi na kumshambulia Mbatia ,CHADEMA na UKAWA
-Wiki ya Tano(Ya nne kwa Kampeni) Ikaibuliwa TWAWEZA na Takwimu in reverse order.
-Leo Siku ya Idd ni Mapumziko, Tuna mkakati wa Wiki ijayo na mingine
ukiwepo ule wa kumshawishi Kiongozi mmoja wa juu wa vyama vinavyounda
UKAWA na ule wa kujaribu kuhonga baadhi ya MaofIsa na wakurugenzi wa
ngazi za juu wa vyama washirika wa UKAWA kufanya uasi
Viongozi wa Dini na makundi maalumu ya kijamii ni miongoni mwa
wanaotarajiwa kuandaliwa matukio hasi yatakayotumika kuchochea chuki
dhidi ya Upinzani wiki nne zijazo kwa mujibu wa mkakati wao kama
kilivyofanya chama tawala cha Nigeria PDP katika wiki za lala salama na
vilevile walivyofanya KANU ya Kenya wiki ya Lala Salama
Tuendelee kubeba ajenda za wananchi na tuwe katika mood nzuri ya
kuunda serikali mpya ya awamu ya Tano kutoka Upinzani kwa mara ya kwanza
tangu tupate Uhuru .
Tuanze awamu nyingine kwa ari zaidi na awamu ya kwanza kwetu ni
fountain of inspiration baada ya kuvunja ngome za CCM katika awamu ya
Kwanza.
Nilipokuwa Mtwara juzi nilipigwa Butwaa kwa Umati Wa Maelfu ya Wakazi
wa Mtwara walioapa Uwanjani kulipiza kisasi kupitia shahada zao juu ya
dhuluma ya Utawala wa CCM katika sakata la Gesi
CCM sasa haina Ngome,Tumevunja Ngome zilizobaki za Lindi na Mtwara.
Unenguaji na push up za mgombea Urais Majukwaani umeshindwa kabisa
kuwashawishi akina Mama wanaotembea kilometa nyingi kuteka maji,Wagonjwa
wanaopata huduma mbovu. Pushup 3 za Magufuli zimeshindwa kabisa
kuwashawishi vijana wasio na ajira na wanafunzi wanaokosa mikopo pamoja
na walimu wanaoishi katika mazingira magumu. Hata kule Nigeria Mgombea
Urais wa Chama Tawala Rais Jonathan aliJitahidi kupanda na nguo za
michezo majukwani na kupiga sarakasi lakini alishindwa kurudisha ngome
zilizotekwa na APC kwa ajenda
Tumefikia pale kilipofikia chama cha APC katika Wiki nne za Kampeni
wakati CCM wanachanja mbuga kupita njia ya PDP iliyoshindwa na UKAWA ya
Nigeria(APC)
Aluta Continua,Victory Ascerta.....
Ben Saanane
0 comments :
Post a Comment