Mbunge aliyemaliza muda wake, Makongoro
Mahanga amewataka wananchi kuachana na CCM kwani viongozi wa CCM wanamapembe
hawataki kufanya kazi kwa kushirikiana, hii yote ni kwasababu ya wizi hasa
madiwani, wakuu wa wilaya na mikoa.
Ameyasema hayo leo kwenye mkutano wa
UKAWA, wa kumnadi mgombea ubunge wa jimbo la Segerea, Julius Mtatiro. Amesema
kuwa yeye anauzoefu kwa viongozi hao kuwa
na viburi hasa katika kushughulikia matatizo ambayo yanatakiwa kushughulikiwa
kwa pamoja hivyo wananchi wasifanye makosa ya kuichagua CCM.
| Mtatiro akiwa na Makongoro pamoja na mgombea udiwani |
“Viongozi wengi wa CCM
wanamapembe na nimabubu, hawataki kushirikiana na wabunge kutatua matatizo ya
wananchi. Madiwani hawataki kumshirikisha mbunge kwenye vikao vyao, wakuu wa wilaya na
mikoa hawataki kutekeleza maombi ya mbunge na hata mameya ndio wanashirikiana
na madiwani kuiba mali za uma. Yote haya nikwasababu ya wizi uliokithiri. Mnataka kumchgua
mgembea ubunge wa CCM kata ya Segerea, wakati alikuwa diwani na hajawahi hata
kutoa hoja kule almashauri, Je, bungeni ataweza ? yeye alikuwa anasusa susa tu na hii ndio sifa ya viongozi wa CCM kutokuwa na hoja” alisema Makongoro.
Alisema yeye amehama na mipango
yote ambayo alianza na Mh Edward Lowassa, ambayo ilikuwa inawahusu madereva
bodaboda kukopeshwa pikipiki kwa riba ndogo na wakina mama kwenye vikoba pia
kupewa mikopo yenye masharti sawa na bure. Alisisitiza kuwa mpango huo ni
endelevu na amemkabidhi Julius Mtatiro na punde tu atakapochaguliwa
atawakabidhi wananchi.
Kwa upande wake Mtatiro alisema
kuwa matatizo makubwa anayoenda kuyatatua endapo atapigiwa kura ya kuwa mbunge
wa Segerea, ni migogoro ya aridhi, ukosefu wa soko, miundombinu mibovu pamoja
na kuhakikisha mikopo inayotengwa kwaajili ya vijana na wakina mama inawafikia
na bila kuwasahau vijana.
“Najua serikali ya CCM
imewasababishia kukosa fedha nyingi sana kutokana na fedha hizo kuliwa na wachache. Mlitakiwa
kupata kila kata zaidi ya miloni 400hadi 500 kwaajili ya maendeleo, na
mlitakiwa kupata milioni 220 kwaajili ya mikopo kwa vijana na wakina mama. Zote
hizo hazijawafikia kwakuwa viongozi wa CCM wamekuwa wakila fedha hizo. Je! milioni 500
haitoshi kujengea masoko na miundombinu ya shule na vituo vya afya na vifaa
vyake? hizi zinatosha kabisa” alisema Mtatiro.
| Mtatiro akiwa na mgombea udiwani kata ya Tabata, Assenga |
Mtatiro amewahutubia pia wananchi
wa kata ya Tabata, ambako aliwaambia wananchi kuwa anajua matatizo ya bodaboda
kuzuiliwa kuingia mjini, tatizo la mitaro na ukosefu wa maji wakati maji
yanapitishwa na mabomba kwenda Masaki wakati ni kazi ndogo tu, ya kuchimba
visima vitakavyo sambaza maji kwa wannchi.
Pia aliwahakikishia wananchi
ahadi ya elimu bure inatekelezeka na wananchi wanatakiwa kuichagua UKAWA ili
kufaidi kuwasomesha watoto wao bure kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu, na
wazazi wausubiri kuhangaikia sare za shule tu.
| Mtatiro akiwa na mgombea udiwani kataya Kinyerezi (Greyson Celestine) pamoja na Makongoro wakitoa elimu jinsi ya kupiga kura |
| Kama kawida yake kila kona ya mtaa, kuwe na sherehe anawafikia na kuwapa elimu juu ya kupiga kura na kumwaga sera |
| Haachi kula nao |
| Wananchi wa Tabata wakionyesha style ya Magufuli ndio nani...? |
0 comments :
Post a Comment