
Dr S Kiria aliyekuwa mkuu
katika kitengo cha IT Tehama kabadilishwa zikiwa zimebaki siku chache za
upigaji kura. Tunajiuliza inakuwaje abadilishwe leo.
Mtamkumbuka
mara nyingi ndie alikuwa akihojiwa na vituo mbali mbali za TV na
wanahabari kuhusu maswala ya BVR na aliweza kujieleza vizuri na kukithi
matakwa ya wanahabari na wananchi kwa ujumla.
Habari kutoka ndani zinasema Dr Kiria amepozwa na kabila lake kwani
yeye ni wa kaskazini. Ivi sasa katika tume ukionekana ni wa kaskazini
unapigwa chini, huo ndio mkakati kutoka Magogoni.
Wanyetishaji
wanazidi kusema hata Jaji Lubuva alikuwa aondolewe kwenye nafasi yake.
Jaji aligoma kuachia ngazi akisema kwanini aondolewe leo wakati siku za
uchaguzi zimebaki chache???. Akawauliza kwanini hawakumwondoa mwaka
jana???
Hayo yote yanatokana na tume ya mwaka huu kutokubali baadhi ya matakwa ya CCM.
Matokeo aliyatoa Makamba na ya jana Twaweza na leo mkurugenzi wa IT
kuondolewa ni jitahada za kuandaa namna ya kuchakachua kura.
Wafanyakazi wengi wa tume wamechanganyikiwa na hawaelewi haya
yanayotokea sasa. Kwani wanasema Kiria alikuwa anaimudu idara yake na
alikuwa mtetezi wa wanyonge.
Chanzo. Julius Mtatiro
0 comments :
Post a Comment