TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749




Mgombea ubunge kupitia UKAWA kwa tiketi ya CUF, Julius Mtatiro amewahakikishia wananchi wa jimbo la Segerea kuwa yeye atakuwa mbunge mwenye silaha nne za kuangamiza matatizo ya wananchi katika jimbo hilo na taifa kwa ujumla.
Ameyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Kimanga, mtaa wa Tembo Mgwaza. Amesema yeye anautofauti mkubwa na wagombea wa vyama vingine, ambao wao hawana sifa hata moja ya aina ya kiongozi ambaye anatakiwa kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazo wakabila wananchi wa jimbo la Segerea.
"mimi ninasiraha nne za kuwapambania nyie wananchi wangu, kwanza ni elimu niliyonayo, pili ni uzoefu wa uongozi ngazi za juu, tatu ni upambanaji kwa ajili ya wannchi wenzangu na nne ni kufanya kazi kwa kuhusisha wananchi na viongozi wangu wa chini" alisema Mtatiro.
Alieleza kuwa elimu yake ataitumia kuleta utawala bora na kuhakikisha anaitumia vyema taaluma yake ya sheria kuwasaidia wananchi wanaohitaji msaada wa kisheria. Aliongeza kuwa uzoefu wake katika uongozi kuanzia akiwa waziri mkuu wa serikali ya mwanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam hadi kuwa naibu katibu wa CUF na kuwa katibu wa UKAWA, atautumia kuongoza wananchi wa Segerea kwa kuwatatulia matatizo yao kama alivyokuwa akiyatatua ya sehemu zote alizopita za uongozi wake.
Aliongea kuwa yeye hajaanza leo kuwapigania masikini na wasaka maendeleo, kwani ameendesha mapambano ya kudai haki ya watoto wa masikini, ya kusoma kwa kupewa mikopo akiwa kama waziri wa mikopo serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam, na akafanikisha hilo, na pia alipambana kuhakikisha katiba ya wananchi inaandikwa kulingana na matakwa ya wananchi akiwa kama katibu wa UKAWA na akiwa mbunge wa bunge maalumu la katiba.
Akielezea siraha yake ya nne alisema kuwa yeye atakuwa mbunge wa kwanza kwa jimbo la Segerea kufanya kazi na wananchi kwa kuwafuata mitaani kwao kusikiliza shida zao kama anavyofanya kwenye kampeni.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Kimanga, John Mjema, alisema yeye anajivunia mafanikio aliyoyapata kwa kuwapigania wananchi katika matatizo mbali mbali kwa kipindi kifupi alichowatumikia akiwa kama mwenyekiti wa serikali ya mtaa, kitu ambacho kimewafanya wananchi wampe ridhaa ya kugombea udiwani.
Amesema, ameshughulikia matatizo kama ya kupata soko la kisasa la Upogoroni, ameanzisha gulio la kila wiki, siku ya jumatano. Pia amesema amesaidia kumwaga vifusi katika barabara ya kimanga kipindi ambacho iliharibika na kuokoa usumbufu ambao wananchi walikuwa wakipata kipindi hicho. Aliongeza kuwa uadilifu, uaminifu na kumwogopa Mungu ndivyo vinamfanya awe mwajibikaji kiasi hicho.
Mtatiro aliwataka wananchi kufanya maamuzi sahihi kwa kuipa kura ya ndio UKAWA kuanzia udiwani, ubunge na urais, ili kufaidi siraha alizo nazo na kutaka mabadiliko ya kweli kuanzia elimu, miundo mbinu afya, amani na upendo pamoja na uchumi wa nchi.
Alisisitiza kuwa wananchi wa Tanzania wanahitaji elimu bure ili kila mtu awe na uwezo wa kusomesha watoto wake na yeye kujisomesha, na hii yote inawezekana chini ya serikali ya UKAWA kwa kutumia malighafi zilizopo na kupunguza matumizi mabovu ya serikali, kama vile safari za rais zisizo za msingi na kukusanya kodi kikamilifu na lutokomeza ufisadi.
Mtatiro akiongea na mama ntilie na kuwajibu jinsi atakavyotatua kero zao



Kijana wa CCM akiikanyaga kadi ya chama chake na kuhamia CHADEMA


Mtatiro akiongea na vijana wa bodaboda na bajaji na kuwaambia jinsi atakavyotatua changamoto zao akianza na kuruhusiwa kwenda katikati ya mji

Yeye anasema kila mtu anakura yake, haachi mtu


Hii ni kero kwa wana Kimanga

Wananchi wanasema kutowajibika kwa viongozi kumesababisha mtalo huu kutozibuliwa baada ya kuzibwa na mtu ambaye tayari ameamliwa na mahakama kuzibua

0 comments :

 
Top