KUTOKANA na sheria ndogondogo kuwa kandamizi kwa wafanya bisashara wadogo wadogo, ifikapo October 27 itakuwa ndio mwisho wa sheria hizo ambazo zimekuwa zikitungwa na madiwani ambao wanakuwa wanatunga kwa maslahi yao wenyewe.
Hayo yamsemwa na mgombea ubunge wa jimbo la Segerea, Julius Mtatiro, alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Mnyamani alipokuwa akinadi sera zake na kumnadi diwani wa kata hiyo na mgombea urais Edward Lowassa, wote kupitia UKAWA. amesema kuwa kuanzia 27 October utakuwa mwisho wa sheria hizo endapo UKAWA itapewa dhamana ya kuiongoza serikali ya awamu ya 5 chini ya Lowassa, mwenye maamuzi magumu na mwajibikaji kwa wananchi na nchi yake.
Ameeleza kuwa kumekuwa na usumbufu kwa mama ntilie, machinga na vijana kukamatwa pasipo na makosa kutokana na sheria mbovu ambazo hutungwa na madiwani wa manispaa au almashauri husika ambao kwa miaka 50 iliyopita, madiwani wengi wamekuwa ni kutoka CCM na hao ndio wamekuwa wakikandamiza kutunga sheria ndogondogo ambazo ni kandamizi kwa wananchi na zeneye manufaa ya wao kujilimbikizia mali na kula pesa za mapato ya manispaa au almashauri.
Amesema kuwa katika jimbo lake la segerea wannchi wategemee kuwa na mbunge mwanasheria ambaye atawaongoza madiwani wake kutunga sheria ambazo zitakuwa na manufaa kwa wananchi na mstakabali wao wa maendeleo.
"Madiwani wa CCM ndio wamekuwa wakiwasumbua kila siku kwa kuwakimbiza na biashara zenu kupitia mgambo, wakiwatoza pesa za ukusanyaji wa taka wakati hakuna kuna bilioni 3 hutengwa kwaajili ya kushughulikia taka. Sasa ifikapo October 25 huu ndio uwe mwisho wa visheria vibovu kama hivi kwa kuipa kura ya ndio UKAWA kuanzia udiwani, ubunge na urais"
Pia ameeleza kuwa sheria hizo ndizo zimekuwa zikisababisha uwizi wa fedha za maendelea ya kata au jimbo na fedha za kuwasaidia wannchi katika kuwawezesha kimikopo na misaada ya kawaida inayohitajika kama vile vifaa vya michezo kwa timu za michezo ndani ya kata husika, kutokana na viongozi wa CCM hushindwa kutunga sheria zinazowabana madiwania na wabunge kuwajibika kwa wnanchi, lakini wananchi wakiichagua UKAWA itatunga sheria hizo na kufanikisha kuwa na viongozi wawajibikaji.
Akijibu maswali yaliyoulizwa na wananchi kuhusu ahadi zake za kuhakikisha ofisi ya mbunge itakuwa na wanasheria, je watalipwa na nani..? Mtatiro alisema kuwa kwanza jimbo la Segerea huwa na gawio kubwa la mapato, hivyo uwezo wa kuwalipa wanasheria hao upo, lakini pia alisema haitakuwa shida kutoa milion 2 au zaidi katika mshahara wake wa milioni 12 kama mbunge. Lakini alitolea ufafanuzi juu ya utoaji wa michango ya mitihani kwa wanafunzi wa darasa la nne, kiasi cha shilingi elfu arobaini alisema kuwa wannchi watambue kuwa ahadi ya elimu bure ni pamoja na kutoa michango yete iliyokuwepo wakati wa serikali ya CCM na hivyo wajibu wa mzazi itakuwa ni kumnunulia mtoto sare za shule tu.
Aliwaomba wannchi kuwa na uchungu wa maisha wanayoishi kwani CCM ndiyo iloyowafikisha hapo walipo kutokana na ufisadi na unyonyaji kwa wananchi uliokithiri, unyonyaji unao wafanya wachache kuwa matajiri kwa mgongo wa kodi wa watanzania huku wenyepesa wakizidi kuwa maskini
zaidi.
zaidi.
0 comments :
Post a Comment