Mtatiro akimuapisha mgombea udiwani kata ya Minazi mirefu, Kasim Mshamu |
Vijana wa kata ya Minazi mirefu, jimbo la Segerea, wamekuwa wakikumbwa na dhahama ya kusombwa na polisi pasipo makosa, pale tu wanapojulikana wanaunga mkono wagombea wa UKAWA ambao ni Kasim Mshamu mgombea udiwani, Julius Mtatiro mgombea ubunge na Edward Lowassa mgombea urais.
Hayo yamelezwa leo na mgombea ubunge wa jimbo hilo, Julius Mtatiro wakati wa kunadi sera zake katika kata ya Minazi mirefu. aliwaonya viongozi wa CCM wanaoratibu hujuma hizo kuwa waache maramoja.
"Namuonya Chitanda pamoja na Ubaya Chuma, waache maramoja kitendo cha kuwaonea vijana wanaotaka mabadiriko kwa kuwakamata kamata bila makosa. Watambue kuwa wao ni wachache lakini vijana ni wengi na wakiamua kuwashughulikia wanaweza" amesema Mtatiro.
Aliendelea kusisitiza kuwa, jimbo la Segerea linahitaji mbunge mpiganaji na mpambanaji kama yeye kwani serikali inahitaji kukumbushwa kila siku kuhusu ahadi zake na kuambiwa matatizo na kero za wananchi zinazohijaka kutatuliwa.
Mtatiro akizindua kijiwe cha CUF |
0 comments :
Post a Comment