TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


KWA mara ya kwanza wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz ametoa kauli baada ya mama yake mzazi, Bi Sandrah kusema kuwa mzee Abdul si baba mzazi wa Diamond.

Diamond akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari kwenye mkutano na waandishi wa habari wa Tunawasha na tiGO, alisme kuwa, katika tukio lililipo kwa wakati huo sio vyema kuyazungumzia hayo mambo, maana sio sehemu sahihi.

"Dada yangu Beatrice nikuambie, kila maneno yanamahala pake, tuikisema tuzungumze maneno ya kitandani hapa, sio sehemu yake" Msanii Diamomd

"Kwa bahati iliyokuwa nzuri hapa ni mahali pa Tunawasha na tiGO. Sasa najua nikishasema hilo swala, kila kitu kitaelekea huko. Nitakuwa na interview yangu hapa kuelekea kwenye tamasha, nitazungumza yote" Msanii Diamond

Diamond aliulizwa swali hilo kuhusu ukweli wa baba yake baada ya kuwepo na maneno ya kutoka kwa mama yake akimkana Mzee Abdul kuwa si baba wa Diamond bali ni marehemu Salum Nyange.

Wakati huo kunamzee mwingine aliyeibuka huko Kigoma akidai pia ni baba yake Diamond ambaye alionyesha na uthibitisho wa mfanano wa mwili na viungo vya mwili kama miguu na kifua. Pia alieleza mfanao wa Diamond na mtoto wake huyo,mzee na mfanao wa kundi la damu la Opostive.

Pia mzee huyo amesema yuko tayari kufanya vipimo vya vina saba (DNA) kuthibitisha alisemalo. ANGALIA LIVE HAPA

0 comments :

 
Top