
Nilikuwa napita barabara ya Kilwa, nikaktana na kundi kubwa la watoto
wakiingia Chuo cha Polisi Kurasini,nilipoulza kulikoni nikaambiwa, ni
halaiki ya watoto wazalendo wakijiandaa na sherehe za Muungano.
Kuwaangalia wote ni watoto wa maskini. Swali la kujiulza, mkuu wa kaya
na Serikali yake, wanajimwambafy kila siku kuwa ni viongozi wazalendo,
tena wengine hadi wanalala na maskafu shingoni yenye rangi za bendera ya
taifa, watoto wao mbona hawashiriki katika hizi halaiki kama kweli wana
uzalendo?
Kwa mtizamo wangu litakuwa jambo la maana sana kama tutamuona
binti wa Kikwete, watoto wa Pinda, Nchemba, Makinda, Komba, na wengineo
wote wanaojiita wazalendo ili watoto wao waige uzalendo huu, vinginevyo
huo ni unafiki tu. Karibuni wadau kwa mawazo, nikosoeni kama siko
sahihi
Chanzo jamii forum
0 comments :
Post a Comment