
Mama maria amtabiria Dk Slaa kuwa kiongozi wa taifa hili mwakani,
Asema CCM inayumbisha nchi,sio wazalendo ...tena
Awapa baraka UKAWA na kusisitiza CCM iheshimu maoni ya watanzania waliowengi,aitaka iache ubabe.
Asema CCM inayumbisha nchi,sio wazalendo ...tena
Awapa baraka UKAWA na kusisitiza CCM iheshimu maoni ya watanzania waliowengi,aitaka iache ubabe.
Dr Slaa alakiwa na Familia ya Nyerere Butiama
Viongozi wakuu wa UKAWA wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chadema Dr Wilbrod Slaa wametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa kijijini Butiama.
Mara baada ya kufika viongozi hao walilakiwa kwa shangwe na wanafamilia ya Mwalimu Nyerere ambapo walikaribishwa kwa mazungumzo mafupi kwenye nyumba aliyokuwa anaishi Mwalimu Nyerere.
Baada ya mazungumzo hayo ya Faragha waliongozwa kwenda katika kaburi la Baba wa Taifa na kuweka mashada ya maua.
Wakizungumza baada ya mazungumzo hayo wanafamilia hiyo ya Nyerere wameungana na UKAWA kutaka maoni ya wananchi yaliyowasilishwa na Jaji Warioba katika Rasimu ya Katiba yaheshimiwe.
Mmoja wa wanaukoo wa Nyerere akihojiwa amesema ni ulevi tu wa madaraka kupuuza maoni ya wananchi na kumtusi warioba.
Source:ITV Habari
0 comments :
Post a Comment