
Waziri wa serikali za mitaa wa Malawi, Godfrey Kamanya amejiua kwa kujipiga risasi kutokana na kile kinachoelezwa ni matokeo mabaya aliyoyapata katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo licha ya kwamba hadi sasa matokeo rasmi hayajatoka. Waziri huyo ameacha maelezo ambayo anamtaka Rais wa Malawi ambaye anawania kurejea madarakani kwa kipindi kingine Joyce Banda, kumuangalia binti yake na kuhakikisha anapata elimu. Msemaji wa waziri huyo amekanusha kuhusishwa kwa kitendo hicho cha kujiua na matokeo ya uchaguzi.
0 comments :
Post a Comment