Wachezaji wa Hispania watalipwa fedha mara mbili ya wenzao wa Brazil na Ujerumani kama watafanikiwa kutetea ubingwa wao wa Kombe la Dunia.
Nahodha Iker Casillas na msaidizi wake Xavi wamekubaliana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Hispania, Jorge Perez kuhusu bonasi watakazopewa wachezaji.
Nchi itakayochukua ubingwa itapata Euro 27 milioni, ikiwa ni ongezeko la asilimia 37, walizotoa Fifa kwa bingwa 2010, na kila mchezaji atapewa asilimia 20 zaidi ya bonasi waliyopewa miaka minne iliyopita.
Upande wa Hispania kila mchezaji na benchi lote la ufundi watapewa Euro 720,000 kama watafanikiwa kutwaa Kombe la Dunia kwa mara ya pili, wakati wachezaji wa Brazil wameahidiwa kupewa Euro 330,000 kama wakitwaa ubingwa huku Ujerumani wakitegemea kuweka kibindoni euro 300,000 kama watanyakuwa taji hilo.
Chanzo Mwananchi
Kiasi hicho cha fedha wanachopewa wachezaji wa Hispania kimezua mjadala nchini humo kwa kuandikwa katika "Twitter":
“Hispania kulipa bonasi mara mbili ya Ujerumani kama watashinda Kombe la Dunia. Sisi ni matajiri mara mbili ya Ujerumani?”
Hata hivyo, Kocha wa Hispania, Vicente del Bosque alitetea jambo hilo kwa kuwaambia wanahabari:
“Tunachotaka sisi kila kitu kitakachofanywa kifanyike kwa uwazi. Ni matumani yetu tutashinda taji hili na malipo yetu yote yafanywe kupitia hazina.”
Chanzo Mwananchi
0 comments :
Post a Comment