TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749



Dodoma. Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM) amejibu mapigo ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisema waziri huyo ni mbumbumbu kutokana na kitendo chake cha kuwasilisha tuhuma dhidi yake bungeni, huku akitaka achukuliwe hatua na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Juzi jioni wakati akijibu hoja za wabunge mbalimbali kuhusu Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini mwaka 2014/15, Profesa Muhongo alisema ana ushahidi wa CD unaoonyesha jinsi Ole Sendeka alivyozungumza na kufanya mambo kinyume na kanuni na maadili ya CCM.

“Nina CD hapa nimeileta ili muipeleke kwenye chama halafu kitapima kama kinataka kuwa na watu wa aina hii. Pia nilidhani ni mtu genius (mtu mwenye akili) na wamenipatia matokeo yake ya mtihani wake wa sekondari,” alisema Profesa Muhongo huku akianza kuyasoma kabla ya kuzuiwa.

Lakini jana Ole Sendeka aliyezungumza na gazeti hili alisema kuwa waziri huyo ni mbumbumbu na hajui kanuni na taratibu za CCM katika suala zima la kuwasilisha malalamiko au ushahidi wa jambo fulani. “Anapeleka CD kwa Spika wa Bunge, kwani Spika ni karani wa CCM? Hajui kanuni za Bunge, wala za CCM.”

Chanzo mwananchi

0 comments :

 
Top