| January Makamba, naibu waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia |
CHAMWITA leo walikuwa na kongamano lililokuwa linajdili changamoto mbalimbali za waimbaji wa nyimbo za injiri nchini Tanzania ambapo mgeni rasimi alikuwa ni Naibu Waziri wa mawasiliano, sayansi na teknolojia Mh January Makamba, huku kukiuzuliwa na wegeni wengine mbalimbali kama vile, Kitime, Pof Mahalu. Lakini pia kulikuwa na wawakilishi kutoka KOSOTA, BASATA, TRA na wasmbazaji wa kazi za nyimbo za injiri: Audio visual na Mwananchi
Wasanii wa nyimbo za injiri walikuwa na malalamiko mbali mbali kwa serikali, KOSOTA, BASATA, TRA, na Wasambazaji wa kazi za nyimbo za injiri.
Akizungumzia matatizo yanayowakwamisha wanamziki katika kupata haki zao, alianza na kupitwa kwa wakati kwa sheria ya hati miliki, kwani haielezi wazi ni wapi zinapelekwa CD ambazo hukamatwa kama ni feki na adhabu inayotolewa kwa anayekamatwa na CD feki ni ndogo, kwani sheria inasema atakayekamatwa na CD feki atalipa faini isiyozidi milioni tano.
"Hii adhabu si sahihi na tena imepitwa na wakati kwa sasa kwani inaposema faini isiyozidi milioni tano, hata elfu tano haizidi milioni tano, kwa hiyo mtu anaweza kukamatwa na akalipa laki mbili tu huku akiwa amekamatwa na mzigo wa CD hata elfu tano" alisema Ado
Pia Ado aliongelea tatizo la TRA kuweka utaratibu mgumu wa upatikanaji wa stemp kwa ajili ya CD original, kwani msanii anapohitaji Stemp toka TRA kwa ajili ya CD anaambiwa ni lazima achukue stemp 5000. alisema kuwa kiukweli hii hailengi kumsaidia msanii bali kumshurutisha msanii.
Rais wa chama hicho hakuwaacha wamiliki ya makampuni ya simu kwani nao ni kati ya wanyonyaji wa kazi za wanamziki katika upande wa nyimbo za miito kwa wateja wanapo piga simu. Akifafanua kiasi wanachopewa wasanii kama malipo ya nyimbo zao na makampuni ya simu alisema kuwa, makampuni yanawalipa wasanii kiasi cha shilingi 3 katika 400 au 300, ambacho alisema ni kiasi kidogo na hakiendani na thamani ya mziki wa wasanii hao na kuyataka makampuni hayo yaongeze hicho kiasi na kufikia walau hata nusu ya gharama wanazo mtoza mteja yaani Sh 200 au Sh 150, huku akitupia kilio kwa Makamba ili amsaidie katika jambo hilo.
Katika vilio hivyo, Bw Ado hakulisahau bunge la katiba mpya kwa kulitupia mbali suara la haki za umiliki wa kazi zao wasanii kwani katika rasimu hakuna jambo hilo ingawa walipeleka mapendekezo yao juu ya jinsi gani katiba inaweza kutambua suara la hatimiliki za kazi za wasanii.
OMBI LAO KWA MH MAKAMBA
Rais wa chama hicho CHAMWITA aliwasilisha maombi yao kwa Makamba ikiwa ni pamoja na, studio iliyo ya kisasa, itakayo wawezesha wanamziki wa nyimbo za injiri kurekodi kwa bei nafuu na kwa ubora wa juu zaidi. Pia walimuomba Makamba kuwafikishia ujumbe wao kwa serikali kuwa wanaomba somo la mziki liwe linafundishwa mashuleni toka ngazi ya shule za msingi, kwani mziki pia ni sekta mhimu inayoweza kuiingizia serikali pato kama kutakuwa na mkazo zaidi na uwezeshaji mzuri, huku akiitolea mfano nchi ya marekani ninavyo nufaika na wasani wa nyimbo mbalimbali
"tulisikia maproduza walioletwa na Mheshimiwa raisi wanavyoingiza kiasi cha pesa na ni jinsi gani wanavyoliingizia taifa lao pato kwa njia ya kulipa kodi, walisema wanaingiza mabilioni ya madola na wanalipa kodi kiasi kikubwa pia" Alisema Ado
| January Makamba akijibu maobi ya CHAMWITA wakati wa kongamano hilo |
MAJIBU TOKA KWA MAKAMBA
Akijibu maombi yao Makamba alisema, suara la studio ni kubwa saana na ni vyema wasanii pia wakatoa nguvu zao katika jambo hilo ili kuwe na uzito kwao katika kuilinda studio hiyo na si kupewa bure tu,
"Mkiipata bure hamtakuwa na uchungu na studio hiyo kwani kila mtu ataona kama sio ya kwake, hivyo ni bora mkachangia hadi mtakapofikia na hapo ndio mniambie ni kiasi gani mmefeli hapo mimi nitamalizia kilichobaki" Alisema Makamba.
Akitoa msisitizo kwa TRA, Makamba alisema kuwa TRA wanapaswa kupunguza idadi ya stemp zinazowekwa kwa wasanii na atahakikisha hilo jambo linatekelezeka.
Kwa upande wa miito ya simu alisema kuwa Wizara itahakikisha kunakuwa na uwazi ya mapato kwa makampuni ya simuy ili wasanii wajue ni kiasi gani wananyonya na hivyo iwe rahisi kwa wao kupata haki yao. Lakini jambo lingine alilo liibua ni kuhusu redio nazo kuanza kulipia kupiga nyimbo za wasanii na si wasanii kuwalipa ma DJ wa redio na TV mbalimbali ili nyimbo zao ziweze kupigwa kwanye stasheni mbalimbali.
Makamba hakuachilia suala la mabadiliko ya teknolojia na hivyo kuwataka Waimbaji wa nyimbo za injiri kuenda na wakati na kuacha kutegemea CD peke yake, wajaribu kuanzisha Player ya nyimbo za injiri kwenye mitandao ya kijamii kupitia internet, na kuahidi kuwasadia kutafuta wataalamu wa jambo hilo na pale watakapo panga kukutana tena atawaleta hao wataalamu ili waonyeshe ni jinsi gani inafanya kazi.
"Hii itawarahisishia mauzo kwani yeyote atakayetaka wimbo wako ataupat online na kulipia huko kwa njia ya M-pesa, Tigo pesa, au benki na hivyo mapato kutopotea kirahisi. mfano mzuri ni Ali kiba alivyozindua wimbo wake hajatoa CD bali amezindua online" Alisema Mkamba.
Makamba ambaye alikuwa ni mgeni rasmi wa kongamano ohilo alionyesha jinsi anavyochukizwa na kitendo cha wasanii wa nyimbo za injili wanavyotengeneza mazingira ya wao kuwa story katika magazeti ya udaku utokana na matendo machafu wanayoyaonyesha kwa jamii na hivyo kushusha ubora wao kwani wao huwa ni mfano mzuri kwa jamii kulingana na ujumbe wanaoutoa
Kwa upande wa Wasanii walionekana kufurahishwa na mwitikio wa Mh Makamba na hivyo kumuahidi kumuombea katiaka michakatoyake yoyote ile ikiwa hasa ile ya kisiasa na kumtaka aendelee na michakato yake na wao wako nyuma yake kwa maombi.
Pia, wasanii waliomba kuwa na jengo la chama chao ambalo litawawezesha kuwa na ofisi za kudumu, hasa wakielekeza maombi hayo pale makamba atakapo pata uraisi. jambo ambalo lilionyesha wazi kuwa wanamuunga mkono kwa uamuzi wake wa kugombea urais.
Akijibu ombi hilo Makamba alisema akifanikiwa kupata wadhifa huo, jambo hilo ni dogo saana na hivyo litashughulikiwa kwa haraka zaidi.
Kongamano hilo lilimalizika kwa maombi ya kumuombea January Makamba aweze kushinda kile anachokiomba kwa wananchi(urais).
| Kitime akimkabidhi vitabu vilivyotolewa na chama |
|
| Picha ya pamoja kwa baadhi ya viongozi wa CHAMWITA na waimbaji mbalimbali |
| Makamba akijibu maswali mbalimbali toka kwa waandishi |
0 comments :
Post a Comment