TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Ndege ya shirika la ndege nchini Algeria imepoteza mawasialiano dakika chache baada ya kupaa angani ikitokea Ouagaougou nchini Burkina Faso mapema hii leo.

Ndege hiyo yenye namba AH5017 ilikuwa na abiri 110 na wafanyakazi 6 huku mashuhuda na watalaamu wa mambo ya anga wanasema ndege hiyo imepoteza mawasiliano kutokana na hali hewa kuwa mbaya.

Ufaransa inasema kulikuwa na  raia 50 ambapo jeshi la nchi linatarajiwa kupeleka vikosi vya uokozi katika eneo la tukio.

Ndege hiyo ilikuwa ikisafiri kutoka Burkina faso kwenda Algeria kupitia jangwa la sahara ambapo watalaam wanasema huenda ndiko ilikopoteza mawasiliano japo duru za habari zinasema ndege hiyo huenda imeanguka kaskazini mwa miji ya Gao na Tessalit iliyoko nchini Mali.

0 comments :

 
Top