TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Zitto Kabwe (CHADEMA)
Zitto Kabwe leo asubuhi alipokuwa akihojiwa na Jerad Hando wa Cluods fm juu ya message ujumbe ambao huwa anatuma kwenye facebook na tweeter, anakuwa anamaana gani kama yeye...?
Jibu alilotoa ni moja tu likiwa bado linautata, alisema  "WATCH MY STEP" na kutotoa ufafanuzi wa hizo step zake.

Kuhusu mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya amesema anaona kunamvutano kati ya UKAWA na uongozi wa Bunge la katiba mpya unaoongozwa na spika wa bunge hili Samweli Sitta.

Alisema sababu kubwa saana inayo wafanya wote waendelee kulumbana ni kwamba hawataki maridhiano baina yao.
"Kwa mfano, UKAWA wanapo kataa wanakuwa hawataki kuukamilisha huu mchakato na upande wa viongozi wakiona UKAWA hawajafika wanasema wataendelea hivohivo." Alisema.

Na kwa busara inabidi huu mchakato usimamishwe kwanza, kwa kuwa inaonekana katiba kupatikana haiwezekani kwa sasa. Inabidi tusubili hadi uchaguzi ufanyike na ndio tuanze mchakato huu tena kuliko kuenda kutumia pesa za wananchi na bila mafanikio, hapo tujue tutakuwa hatujawatendea haki Watanzania.
"Tuchukue mfano wa Baba wa taifa Mwalimu J.K Nyerere alikuwa akiona jambo halijafanikiwa, alikuwa anasubili na kutoa mda kwa kila upande mpaka hapo jaziba zitakapo isha," Alisema Zitto

Kikubwa cha kuzingatia ni kufanya baadhi ya mabadiliko katika katiba hii ya sasa ili iweze kusimamia uchaguzi wa haki na kweli na baadhi ya hayo mabadiliko ni kama vile

-Suala la mafuta na gesi lisiwe la muungano, Zanzibar waachiwe nao waweze kugawa vitaru vya gase na  mafuta na kusimamia wao wenyewe.
-Kitu kingine ni kuwe na tume huru ya uchaguzi
-Na jambo lingine ambaloliingizwe ni suala la mgomnea binafsi, mtu aruhusiwe kusimama kama mgombea binafsi katika uchaguzi ujao.

Kuhusu ujio wa UKAWA na kama ujio wao ni wa kudumu hadi 2015 katika uchaguzi, Zitto amesema Watanzania wanapenda kuona upinzani wenye nguvu na wananchi ndio wataona ni nani atakayepewa dhamana ya kuongoza nchi kwa kuangalia kukabiliana na  ubadhilifu wa fedha, kuleta maendeleo na kujali Watanzania wenyewe.

Zitto alisema haamini na hana uhakika kama ukawa ni endelevu au ni ya mda tu kwani si mara ya kwanza wapinzani kuwa na maadhimio ya kuungana, huwa kila wakitaka kuungana huwa wanafikia kutokuelewana wakati uchaguzi unakaribia, kwani mvutano huwa unakuwa kwenye nani aweze kupeperusha bendera katika mbio za urais.

"mvutanoi wao huwa ni nani aweze kugombea ngazi ya urais, kila chama huwa wanataka kusimamisha mgombea wao, hapa ndipo kutokubaliana huanza." Alisema Zitto.

0 comments :

 
Top