TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Clara Mwatuka Mbunge aliyedaiwa kujiandikisha Bungeni kwenye Bunge Maalum la Katiba, alitoa Maelezo
Mkurugenzi wa Habari Mahusiano ya Ummaakuna, Abdul Kambaya Naibu amekanusha uvumi uliotolewa kuhusu Mbunge wa CUF kuhudhulia vikao vya Bunge la Katiba Dodoma.
Amesema kuwa hakuna hata mjumbe mmoja wa Chama Cha Wananchi Cuf aliyepo DODOMA kwenye Bunge la Katiba na kusema kuwa hii inatokana na utiifu wa wabunge wao katika misimamo waliyo nayo.
"Tumejijengea heshima kubwa kwa kuheshimu maumuzi ya vikao pengine kushinda vyama vingi Barani Afrika" Alisema
"Hatujaanza leo tumekwisha wazuia wawakilishi kuingia katika baraza la wawakilishi kwa miaka 5 na hakuna aliyeingia pia tuliwazuia wabunge watu kwa miaka wili kuingia bungeni hawakuingia".
MBUNGE WA CUF ALIEDAIWA KUONEKANA BUNGENI
Clara Mwatuka Mbunge aliyedaiwa kujiandikisha Bungeni kwenye Bunge Maalum la Katiba, alitoa Maelezo yake mbele ya Naibu Katibu Mkuu Cuf Magdalena Sakaya. Maelezo hayo ameyatoa Jana Ofisi Kuu Dar Es Salaam.
Kwa mujibu wa mbunge huyo alisema kuwa, Dodoma kunakijana wake anasoma kwahiyo alipitia bungeni kuulizia baadhi ya mabo yake mwenyewe na fasta kunawatu wakampiga picha na kuanza kusambaza kuwa yeye amekwenda bungeni kujiandikisha kama mbunge atakaye hudhulia vikao vya bunge la Katiba.
NB Ikumbukwe kuwa theluthi mbili iko mikononi mwa Cuf na chama hiki nichama makni sana.

0 comments :

 
Top