MAMIA YA WAFUNGWA WATOROKA GEREZANI
Kundi lisilo la kijeshi, limevamia na kuvunja gereza la wafungwa lililoko Haiti na kusababisha mamia ya wafungwa kutoroka, huku kumi wakiwa wamekamatwa na kurudishwa tena gerezani.
Akieleza mkasa huo msemaji wa polisi nchini humo Gary Desrosiers amesema kuwa hakuna idadi ya uhakika ya wafungwa waliotoroka kati ya wafungwa mia nane tisini na tisa, Pia ameongeza kuwa walinzi wawili wamejeruhiwa katika mapigano na kundi hilo.
Desrosiers amesema kuwa chanzo cha kuvamia gereza hilo ni kutaka kumuokoa mfanya biashara mmoja aliyetambulika kwa jina la Clifford Brandt aliye hukumiwa tangu mwaka 2012 kwa kosa la kuwabaka watoto wawili
Polisi wamesema juhudi za kuwatafuta wafungwa waliotoroka zinafanyika na zawadi ya dola za kimarekani elfushirini (20,000) zitatolewa kwa atkaye toa taarifa ya kumpata Clifford Brandt
0 comments :
Post a Comment