WIMBI la unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto walio chini ya umri wa miaka kumi na nane (18), limeendelea kuutikisa mkoa wa Kilimanjaro baada ya Baba mzazi wa mtoto mwenye umri wa miaka minne, kumcharaza viboko mwanae katika sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo chake muda mfupi na kisha kutokomea kusikojulikana mkoani Kilimanjaro.
Katika tukio hilo lililotokea Agosti 10, 2014 ambapo mtoto Nikolaus Morisi (04), mkazi wa Kijiji cha Kanji, Tarafa ya Kirua Vunjo, katika wilaya ya Moshi-vijijini, mkoani humo alikutwa akiwa amekufa pembezoni mwa nyumba waliyokuwa wakiishi baada ya kuchapwa fimbo na Baba yake mzazi aliyejulikana kwa jina moja la Moris.
Taarifa zilizoifikia izzy tz kutoka mkoani humo zinasema, tukio hilo lilitokea saa 11:15 asubuhi, ambapo mtoto huyo alikutwa na mauti baada ya kupata adhabu kutoka kwa baba yake mzazi ambaye alimuumiza vibaya katika mkono wake wa kushoto, makalio pamoja na sehemu mbalimbali za mwili wake zikiwa zimeharibika vibaya.
Majirani wameiambia FikraPevu kuwa mtoto huyo alikuwa akiishi na baba yake pamoja na Mama wa kambo, aliyetajwa kw ajina la Laghtness Willium, (29) ambapo sasa bado haikujulikana chanzo na kosa alilofanya mtoto huyo hadi kupelekea kupatiwa adhabu iliyomsababishia kifo chake.
Jeshi la polisi mkoani humo limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo limesema mara baada ya mzazi huyo kufanya tukio hilo alitokomea kusikojulikana na kuwa Jeshi hilo limeanza msako wa kumtafuta mtuhumiwa ili kumchukulia hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Kilema iliyopo mkoani humo kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Aidha, katika tukio jingine Jeshi la Polisi mkoani humo, linamshikilia, Christofa Nestori (25) mkazi wa mjini humo, kwa kosa la kumpiga fimbo ya kichwani Baba yake mzazi, Nastori Christian (60), na kupelekea kifo chake wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Huruma iliyopo Rombo- Mkuu, katika Wilayani Rombo mkoani humo.
0 comments :
Post a Comment