
Tayari chuo kimepokea cheki leo hii na maandalizi ya malipo yamekamilika. Cheki imepelekwa benki mchana huu na kuna uwezekano watu wa CRDB wakapata pesa yao leo leo.
Kwa wale watakaokuwa na matatizo ya boom wasisite kuwasiliana na waziri wa mikopo kwa muda wowote.
Tuwajulishe wenzetu pesa itakapoingia kwani kuna wengine wapo vijijini kiasi kwamba ni vigumu kuelewa kama pesa imeingia au la.
Nawatakia utekelezaji mwema wa majukumu lakini pia poleni kwa maumivu tuliyoyapata kwa wakati wote huo nikiwemo na mimi.
Mwl. Y.M. Lulyeho.
WAZIRI WA MIKOPO DARUSO-DUCE.
0 comments :
Post a Comment