
Jiji la Dar es salaam liko mbioni kufunga kamera maalumu kwaajili ya kuchunguza uhalifu na makosa mengine yanayoendelea mitaani na barabarani kwa ujumla.
Ufungwaji wa kamera hizi za CCTV itaenda sambamba na kuruhusu watu binafsi kuomba kuunganishwa ili kuunganishwa na mfumu huo utakaokuwa unasaidia kwa ulinzi.
Mfumo huu umeletwa kama mwarobaini wa uarifu na uvunjaji wa sheria za barabarani iliokithili jijini Dar es salaam
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa jiji la Dar Es Salaam, Wilson Kabwe amesema zitaanza kufungwa rasmi mwezi wa saba au wa nane.
Kwa unavyodhani, kamera hizi zitaweza kupuguza uhalifu jijini Dar es Salaam au zitaibiwa zenyewe?
0 comments :
Post a Comment