Umoja wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya wananchi UKAWA leo
umetangaza rasmi kususia vikao vya bunge vilivyobaki kwa madai ya
kukiukwa kwa kanuni za bunge.
Akitangaza msimamo huo mjini Dodoma
katika mkutano na waandishi wa habari, kiongozi wa kambi rasmi ya
upinzani bungeni Mh. Freeman Mbowe amesema wabunge wote kutoka katika
vyama vinavyounda umoja huo hawataingia tena bungeni licha ya baadhi yao
kuwa hawajaadhibiwa.
Wakati huo huo Bunge mchana huu limepitisha miswada miwili iliyokuwa imebaki baada ya mmoja kupitishwa jana.
miswada iliyopitishwa leo ni wa sheria ya usimamizi wa mapato
yatokanayo na gesi na mafuta pamoja na muswada wa sheria ya uwazi na
uwajibikaji katika uchimbaji bila ushiriki wa wabunge wa upinzani.
0 comments :
Post a Comment