TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Nimekuwa nikiona mijadala mingi kupitia mitandao ya kijamii hasa whatsapp,instagram,Facebook,Jamiiforums na blogs nyingi kwa mda wa wiki nzima sasa tangu tr 23/8 mpka leo kuna maneno yamekuwa maarufu sana ingawa inaaminika kuwa maneno haya ni MATUSI(SI MAZURI )KUYATUMIA...Baadhi ya watu wamekuwa wakisalimiana kwa majina haya kuonyesha ni jins gani hawajafurahia kuambiwa maneno haya lkn hawana budi kuyatumia ili kukumbushana kwamba waliitwa hivyo.....binafs nachukulia hii kuwa kama ni mtaji mdogo wa kisiasa kwa ajili ya kujipatia kura za huruma na kweli zitapatikana....na ni halal zipatikane maana waliyataka wenyewe...
Maneno "MPUMBAVU"NA "LOFA" yamejuzulia umarufu mkubwa kipindi hiki cha kampain za uchaguzi mkuu na kwangu mimi naona kama ni misamiati ambayo itakuwa ya kudumu hadi kufikia uchaguzi mkuu kufanyika 25/oct
maneno haya yalitumiwa na rais wa awamu ya tatu mh.BENJAMIN WILLIAM MKAPA(BWM) aliposimama kuongea kwenye viwanja vya JANGWANI wakati wa uzindizi wa kampain za uchaguzi ndipo aliposema**"vyama vinasema vinatafta ukombozi ni wapumbavu na malofa kwa kuwa ukombozi wa Tanzania ulishafanywa na TANU pamoja na ASP**"lakini kauli hii ya mkapa sitaki kuamini kuwa alikuwa anawakashafu UKAWA kwa kuwa UKOMBOZI wa Tanzania na Africa haujakamilika mpaka leo na hata CCM walitakiwa waendelee kuhubiri kwamba wanatafta ukomboz wa tanzania mana  haujalamilika.....na inawezekana hautakamilika leo au hata kwa zaidi ya miongo mitatu ijayo"ukombozi ni ongoing process'not an overnight process".
Kamusi ya kiswahili sanifu(1982:298)inasema"ukombozi ni uokoaji wa watu toka kwenye hali mbaya au udhalimu"na kwa tafsr hii basi ukomboz wa tanzania bado haujakamilika maana hali.mbaya,udhalimu havijaisha katika jamii hii,katika kizazi hiki ukombozi bado unahitajika tena kwa nguvu zaidi kuliko kipindi chote kilichowai kupita maana Taifa lipo katika hali mbaya zaidi katika kipindi hiki.
Ukombozi kama ni kuondoa katika hali mbaya ,basi Tanzania bado tupo kwenye hali mbaya.....kila secta ipo katika hali mbaya..........
viwanda vimekufa''''vinahitaji ukombozi toka kwa watu walio tayari kuufanya ukombozi
shule hazina madawati"""ukombozi unahitajika juu ya hilo..
Hosptali hazina dawa ukombozi unahitajika ili kuikoa jamii hii....
walimu wanalalamika mishahara haitoshi ukomboz ni wa mhimu kwa hili...
UDHALIMU maana yake ni kuoneana na kutesana na kama ni hivyo basi ukombozi dhidi ya udhalimu ni mhm kwani polisi bado wanaonea raia bila sababu za msingi na pengne kuua watu(rejea matukio ya mauaji kama arusha,iringa,morogoro)hivyo udhalimu bado upo na ukombozi unahitajika....Bado kuna udhalimu kwa ofs za umma watu wakizitumia kama zao (tunahitaji ukombozi kwa hili)
Naomba nimkumbushe tu mkapa kwamba asisahau kwamba ukombozi wa Tanzania bado unaendelea kwani hali ya nchi bado ninya kutisha sana....siyo tu kutisha balo hali ni dhohofu....
Tulipopata uhuru kila mtu alitaka maendeleo na kama ni maendeleo basi mapaka sasa hatuwezi sema tumeyapata...
Mwandishi na mwanaharakati walter roodney alipata kuandika maana ya maendeleo katika kitabu chake maarufu"HOW EUROPE UNDERDEVELOPED AFRICA"alisme"DEVELOPMENT in the past has always meant the increase in the ability of social group and indeed to infringe upon the freedom of others"....so if development is to increase freedom tanzania still needs a real transformation and BWM to say it is done was totally wrong and still it is wrong .....in contrary walter roodney came with a definition of UNDERDEVELOPMENT where by he said "underdevelopment is not absence of development  because every people have developed in one way or another and to great or lesser extent.It makes sense only a means of comparing levels of development" apparently here the hero walter was talking about maendeleo yanapaswa kusemwa maendeleo kama tu tutalinganisha na sehem zingine,mda uliotumila kuyapata na hata rasilimali zilizotumika kuyaleta na kwa kuangalia haya nakubaliana na wengi kwamba safari iliyotumika kufikia maendeleo yaliypo leo tanzania haviendani na hivyo kwa neno fupi we are not developing but underdeveloping since the resources used to bring us here is not equivalent to the development we have that we call underdevelopment and we need liberation"UKOMBOZI"na kwa hilo MKAPA hakuwa sahihi kusema kwamba wanaosema kwamba wanatafta ukombozi wa TANZANIA ni wapumbavu na malofa maana ukombozi haujakamilika na utakamilishwa na wengi si CCM peke yao maana hawana hati miliki ya taifa hili....
ROME WAS NOT BUILT IN A SINGLE DAY...
pole BWM kwa kutokujua maana ya UKOMBOZI na kama ulijua basi toka utuombe radhi watanzania.

0 comments :

 
Top