TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


LEO mgombea wa urais kwa tiketi ya CHADEMA kupitia UKAWA, ameongea na wanawake wa CHADEMA pamoja na wanawake wenzao wa UKAWA, katika mkutano wa BAWACHA uliofanyiaka leo jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Millennium tower.
Akiwa na mgombea mwenza Haji Duni, pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa UKAWA, Lowassa alieleza furaha aliyonayo kukutana na wanawake na kuongea na wanawake wa Tanzania nzima kupitia vyombo vya habari.
Akielezea furaha aliyonayo alisema kuwa kujitokeza kwa wingi kwa wanawake hao ili kumuelezea matatizo yao ni sawa na ushindi kwakuwa wanawake ni ishara ya ushindi, kwakuwa wao ndio wenye matatizo zaidi kwa kipindi cha miaka 50 yote chini ya serikali ya CCM.
Pia alifurahishwa na maneno ya mke wake aliyoyasema kuhusu yeye kuwa ni mchapakazi, mwadilifu, mwenye utu na mpenda maendeleo.
Alieleza umhimu wa wanawake katika mabadiriko, kwani wanawake ndio wanye maamuzi magumu na wanauchungu na matatizo yanayowkumba kila siku.
Aakiwakabidhi kazi kubwa ya kuifanya wanawake katika kipindi hiki cha kampeni na hata siku ya uchaguzi ni ushiriki wao mkubwa wa ushawishi.
"wanawake ni waaminifu na wanamisimamo katika ahadi zao. Kuwashawishi wanawake ni kazi sana, tofauti na wanaume ambao akidanganywa kidogo du anaweza kubadilika. Hivyo wanawake ni hadhina kubwa sana na mnatakiwa kufanya kazi moja kubwa ya kushawishi wengine kuichagua UKAWA na na nyie wanawake wa UKAWA mtunzi vitambulisho vya kupigia kura" alisema Lowassa
Pia alieleza kuwa mabadiliko kwa sasa ni lazima kwa ni hata baba wa taifa alisisitiza jambo hilo na kuonya kuwa, watanzania wasipoyapata ndani ya CCM watayapata nje ya CCM na hivyo aliwataka wale wote wanaotafuta mabadiliko wajiunge na UKAWA kwani, maisha ndani ya UKAWA ni safi.
Kwa upande wake mgombea mwenza Duni Haji, alisema kuwa yeye anaguswa saana na matatizo ya kina mama, hivyo anawaomba wanawake wote Tanzani bara na Zanzibar, kuwaamini UKAWA na kuwachagua ili wawasaidie kupata haki zao.
Mwenyekiti wa CHADEMA aliwapongeza watanzania, hasa wanawake kwa ujasiri wao wa kutoa tofauti zao za kiitikadi, kidini, kikabila na kuungangana pamoja kudai mabadiliko.
Alisema kuwa Lowassa ni chachu ya mabadiliko, ingawa wao na wengine wengi wameanza safari ya mabadiliko tangu 1995, na mpaka sasa wengi wamekumbwa na mambo mengi saana wakipigania mabadiliko hayo.
Lakini pia aliwahakikishia wakazi wa Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla, kuwa uzinduzi wa kampeni siku ya jumamosi tarehe 29/08/2015, uko palepale na hivyo wajitokeze kwa wingi.
"Tulikuwa tunakwazwa na kunyimwa kw uwanja wa Jangwani kuufanyia kampeni, lakini tatizo hilo limeshughulikiwa na hivyo uzinduzi uko palepale. Pia  nimegundua kitu kimoja, wanawake hawapendi misongamano na usumbufu, hivyo natoa agizo kutengwa kwa eneo la kukaa wanawake tu, na red guard msimaie hilo na itakua hivyo kwa kampeni zote zitakazofanywa na UKAWA kwa nchi nzima" alisema Mbowe
Naye Mbatia alisema wakina mama wananyanayasika saana na kulalamika saana kwa serikali ya CCM, lakini hawajawahi kupatiwa ufumbuzi. Alieleza kuwa wakina mama haohao ndio wanaoitwa wapumbavu na malofa kwa kuwa wanataka mabadiliko. Lakini aliwataka wanawake kukumbuka maandiko ya biblia yanayosema kuhusu watu wasio na busara.
"Mhubiri 4:3 inasema hivi, Heri kijana masikini mwenye hekima, kuliko mfalme mzee mpumbavu ambaye hasikii tena maonyo" alieleza Mbatia
Pia aliwataka watanzania kuwapuuza wanaoipinga UKAWA kwani wao ndio wanaoeneza vitu ambavyo sio vya msingi na si vya kulijenga taifa.
"Wakati wao wanahubiri chuki, sisi tunahubiri amani, wakati wao wanaubiri utengano sisi tunahubiri umoja, wakati wao wanahubiri vurugu sisi tunahubiri utulivu na amani" alisema Mbatia
Mkutano huo ulivunja rekodi kwa kuhudhuliwa na wanawake wengi kiasi cha ukumbi kutotosha hali iliyolazimisha screen kutol.ewa nje ili wengine wakae nje na kusikiliza kinachoendelea.

0 comments :

 
Top