TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Shirika lisilo la kiserikali la Save Vulnerable Foundation(SVF) kupitia Baraza la Sanaa , limeandaa tamasha la MLIMBWENDE WETU (MISS ALBINO), Shindano hilo linatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Shindano hilo litakalofanyika kwa mara ya kwanza likiwa na dhumuni mahsusi la kuibua na kutambua vipaji, kujenga ujasiri, kuwawezesha kufikia malengo yao kwa kuwaongezea nguvu, kuwawezesha kiafya, kiuchumi na kielimu linatarajiwa tarehe 04/09/2015 kuanzia saa kumi na mbili jioni nakuendelea. Abapo namna ya ushiriki ni ile ya mwongozo wa Sanaa kutoka Baraza la Sanaa Tanzania, mshiriki atahitajika kuwa na vigezo vinavyoendana na sheria za ushiriki, urefu, uelewa urembo jinsia na namna ya kujieleza utambuzi na pia mshiriki awe ni Mtanzania ambaye hajawahi kuwa na hatia kesi ya jinai wala kashfa yoyote ya kimaadili au kikazi. kuutakuwa na wabunifu wa kitaifa na kimataifa kwa ajili ya uvishaji wa walimbwende, kutakua na waalimu kutoka BASATA na wengineo kwa minajili ya kuwafunda walimbwende namna stahiki nya ushiriki na namna ya kuenenda na kitaalamu hatimaye kumboresha mlimbwende kuenenda na sambaza na sheria za shindano. Wanatarajia kuwa kuwa na walimbwende 12 toka Dar es Salaam, watakaoshindanishwa hatimaye kupata 3 bora na mwisho kumpata mlimbwende  atayebeba taji la mkoa wa Dar es Salaam . Zawadi zimeandaliwa kwa washindi kuanzia 3 bora na mshindi wa jumla sambamba na hilo kutakuwa na uchangishaji wa fedha kwa ajili ya kujenga jiko na maktaba katika shule ya watoto wenye ulemavu wa aina zote pamoja na Albino kilichopo Buhangija, Shinyanga. lengo ni kumpata Miss ALBINO ambaye atawakilisha na  kuwa sauti kuhusu matatizo yao(albino) na kushiriki Miss Tanzania. Ambapo Miss Tanzania 2014 Lilian Kamazima na mamiss wengineo wa zamani watakuwepo.

0 comments :

 
Top