Bingwa wa dunia wa mbio za kufukuza upepo za mita 100 kwa upande wa wanaume,Usain Bolt wa Jamaica, ameibuka na kuwapiku wapinzani wake wakuu alipohifadhi taji lake la dunia mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kushuhudia fainali hiyo katika uwanja wa kimataifa Birds Nest jijini Beijing huko China.
Bolt alitoka nyuma na kuukata utepe katika fainali iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi zaidi katika mashindano ya riadha duniani yanayoendelea nchini China.Raia wa Canada, Andre de Grasse na Mmarekani Trayvon Bromell walitia nanga muda wa sekunde 9.92 na kutunzwa medali ya shaba.
Gatlin alikuwa na rekodi ya kushiriki mbio 28 bila ya kushindwa msimu huu na japo alikuwa amepigiwa upatu kuibuka mshindi huko Beijing,Kulikuwa na hofu kubwa yakuwa endapo angeibuka mshindi basi ushindi wake ungelitia doa jina la mchez o wa riadha ambao umekumbwa na madai hivi majuzi ya matumizi makubwa ya madawa za kuongeza nguvu yaliyopigwa marufuku.
Bolt atakumbukwa kwa kuibuka kidedea kati8ka mbio za matimko alipozoa medali za dhahabu katika mbio za mita 100 na mita 200 katika mashindano ya olimpiki mwaka wa 2008 huko huko Beijing.
Bingwa wa dunia wa mbio za kufukuza upepo za mita 100 kwa upande wa wanaume,Usain Bolt wa Jamaika, ameibuka na kuwazidi wapinzani wake wakuu alipoibuka na taji lake la dunia mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kushuhudia fainali hiyo katika uwanja wa kimataifa Birds Nest jijini Beijing huko China.
Bolt alitoka nyuma na kuukata utepe katika fainali iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watu wengi zaidi katika mashindano ya riadha duniani yanayoendelea nchini China.Raia wa Canada, Andre de Grasse na Mmarekani Trayvon Bromell walitia nanga kwa muda wa sekunde 9.92 na kutuzwa medali ya shaba, Gatlin alikuwa na rekodi ya kushiriki mbio 28 bila ya kushindwa msimu huu na japo alikuwa amepigiwa upatu kuibuka mshindi huko Beijing, ambapo kulikuwa na hofu kubwa yakuwa endapo angeibuka mshindi basi ushindi wake ungetia doa mchezo wa riadha ambao umekumbwa na madai hivi majuzi ya matumizi makubwa ya madawa za kuongeza nguvu yaliyopigwa marufuku.
Bolt atakumbukwa kwa kuibuka kidedea katika mbio za kukimbiza upepo alipoibuka na medali za dhahabu katika mbio za mita 100 na mita 200 katika mashindano ya Olimpiki mwaka wa 2008 huko huko jijini Beijing.


0 comments :
Post a Comment