Jumla ya vijana 91 wamejiunga na chama cha CUF leo katika na kuanza rasmi safari ya kupambana na CCM kwa kile walichokiita kuchoshwa na utapeli wao wa kila siku. Tukio hilo limetokea leo katika mkutano wa kunadi sera kwa mgombea ubunge kupitia UKAWA, Julius Mtatiro na mgombea udiwani kupitia UKAWA, Omary Said.
Wamesema kuwa kati ya mambo waliyoyachoka ni pamoja na maji ya kuletwa na magari, ambayo yanakuwa ya gharama kubwa, wakati nchi hii inamaji mengi chini ya aridhi na kunauwezekano wa kuchimba visima ambavyo vinaweza kutatua tatizo la maji kwa jiji la Dar es samaam.
Waliongeza kuwa CCM imeuza maeneo mengi sana ya wazi ambayo yalikuwa ni tegemeo kwa vijana kwaajili ya michezo na mambo mengine ya kimaendeleo kama vile mikutano.
Mtatiro alisema kuwa uhuni uliokuwa ukifanywa na serikali ya CCM umefikia mwisho kwani mabadiriko yanakuja kupitia UKAWA, na yeye akiwa mwanaukawa amejipanga kutokomeza uhuni wa CCM kwa kuhakikisha wananchi wa kata ya Vingunguti na Segerea nzima wanapata huduma ya maji, huku akiahidi komputa 10 kwa sekondari ya Vingunguti punde tu atakaposhinda uchaguzi. Alisema kuwa, atakapokuwa mbunge ataanzisha maktaba ya jimbo la Segerea, itakayokuwa na vitabu vyote vinavyohitajika kwa wanafunzi na komputa kwaajili ya wanafunzi kutafuta vitabu vingine kwenye mitandao.
Aliongeza kuwa yeye na serikali ya UKAWA ndio tumaini pekee la kurudisha maeneo ya wazi yaliyouzwa na kuhakikisha bonde la msimbazi linawekwewa mawe ili kulilinda. Pia alitoa ufafanuzi wa jinsi gani wanafunzi wanaweza kusoma bure kama sera za UKAWA zinavyosema.
"Tumepiga mahesabu, tukisomesha wanafunzi wato Tanzania nzima, itagharimu kiasi cha bilioni 960, na gharama hiyo CCM wanasema haiwezekani wakati mlima Kilimanjaro tu, unaweza kusaidia kulipa gharama hizo. Mlima kilimanjaro unaingiza kiasi cha bilioni 800 na hapo ni baada ya CCM kuiba, tunaongezea bilioni 160 tu hapo ili kupata bilioni 960. na hizi pesa zitapatikana zaidi kwasababu serikali ya UKAWA itakuwa inasimamia vyema mapato ya wananchi, tofauti na CCM ilivyokuwa ikiwaibia"
Aliongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuwa na wabunge wapiganaji kama yeye na si wabunge wa CCM kwani wamezoea kuunga mkono hoja tu, na hawawezi kujadili kiundani, kutetea walichokiahidi na kuwapigania wananchi katika kila jambo na uonevu wanaokumbana nao.
Kwa upande wake mgombea udiwani wa kata ya Vingunguti kupitia UKAWA, Ommary Said, amesema kuwa yeye ameamua kugombea udiwani kwakuwa anataka kuboresha miundombinu ya shule ya Vingunguti kwa kuhakikisha inakuwa na maktaba nzuri na kurejesha maeneo yote yaliyopolwa na diwani aliyemaliza mda wake kupitia CCM.
0 comments :
Post a Comment