Mgombea ubunge jimbo la Segerea, kupitia UKAWA Julius Mtatiro, amawaomba wananchi kufanye mabadiriko ya kuikataa CCM na kuipa nafasi UKAWA, kwani hata viongozi wadogo wa ngazi za udiwani na umeya ni wezi kama walivyo viongozi wa ngazi za juu.
Amesema kuwa CCM ni sawa na ukoo wa panya kwani babu, baba na mtoto wote ni wezi, hakuna mdogo wala mkubwa. Alieleza kuwa kwa viongozi wa CCM hasa wabunge na madiwani, kuwaibia wananchi ni suala la kawaida na hawana aibu kuiba kweupe huku wakiendelea kujinufaisha wao na familia zao, ndio maana diwani au meya wa CCM utamkuta anamiliki majumba na magari ya thamani wakati kwa kawaida bila kuiba haiwezekani kumiliki vitu kama hivyo ndani ya miaka mitano ya uongozi.
Aliyasema hayo alipokuwa akihutubia wananchi wa kata ya Bonyokwa jimbo la Segerea mkoa wa Dar es salaam jana. Alisema kuwa matatizo mengi sana yanayozikumba kata na majimbo yangeweza kutatuliwa hata kwa mapato na mgao wa bajeti ya serikali kwani ni pesa nyingi sana hutolewa kwa maendeleo ya kata zilizoko ndani ya kila jimbo. Lakini yote hayo hayawezekani kwa sababu ya wizi wa viongozi wa manispaa, hasa manispaa ikiwa na madiwani wengi wa CCM.
Akitolea mfano wa ujenzi wa zahanati ya Kipawa iliyo katika manispaa ya Ilala, Mtatiro alisema kuwa wizi mkubwa ulifanyika wa zaidi ya milioni 110, kwani viongozi walidai kuwa zahanati ilijengwa kwa kiasi cha shilingi milioni 140 wakati zahanati ina thamani ya milioni 30.
Pia alifafanua jinsi CCM inavyotumia vikundi vya vikoba kuwalaghai wananchi hasa kipindi hiki cha uchaguzi kwa kuwakopesha pesa ili wawachague huku nao vijana wakiwa wanadanganywa na jezi za jogging ambazo zina thamani ndogo kuliko kiasi kinachotolewa na serikali kusaidia michezo katika kila kata.
"Kila kata ya manispaa ya Ilala ilitakiwa kupata milioni 30 kwa ajili ya kusaidia michezo, ikiwa ni kununua jezi na mipira kwa timu za kata na zingine zitakazotengenezwa ndani ya kata hiyo, Je mumewahi kuambiwa hilo ? Lakini pia kama wanatambua thamani ya vikoba walikuwa wapi tangu mwanzo kutoa kiasi cha milioni 120 kwa vijana na milioni 120 kwa akina mama, ili kuwakopesha kwa mashariti na riba nafuu kama inavyotakiwa pesa hizo kutumika.? ziko wapi pesa za maendeleo kwa kila kata ambazo hutengwa kutokana na mapato ya manispaa na mgao unaotokana na bajeti ya serikali ambazo kwa ujumla ni karibu bilioni 100. Hamzioni ni kwa sababu ya wizi wa viongozi wa CCM" alieleza Mtatiro
Kwa upande wake mgombea udiwani kupitia UKAWA kwa tiketi ya CHADEMA, Charlees Kweyeko aliwataka wananchi kutofanya makosa kwani kata ya Bonyokwa imesahaulika sana kwa kipindi hiki cha uongozi wa CCM, alisema kuwa barabara na maji ni changamoto kubwa sana katika kata hiyo, lakini pia alifafanua ukosekanaji wa maji, shule na zahanati ndani ya kata hiyo, hivyo kufanya wananchi wa Bonyokwa kutokuwa na miundombinu ya usafiri ya uhakika, huduma za afya za uhakika, maji ya uhakika, na wanafunzi kufuata shule maeneo ya mbali na kata hiyo.
Wananchi wa eneo hilo walisema kuwa wameichoka serikali ya CCM kwani imekuwa haiwathamini kwa muda wa miaka yote iliyopita na sasa ni wakati wa kufanya mabadiriko ili kujaribu kukipa chama kingine na waone watafanya nini kwao.
Akiongea na mwandishi wetu mama mmoja ambaye alikataa kujitambulisha jina lake kwa kuwa ni mfanya kazi serikalini, alisema kuwa Bonyokwa ina tatizo la muda mrefu la barabara ya kutoka Segerea kuelekea Bonyokwa kwani kipindi cha mvua huharibiwa na maji na serikali bado haina msaada wowote kwao na ndio maana wote Bonyokwa wanataka kufanya mabadiriko.
Ni nyumba kwa nyumba kampeni za Mtatiro katika kila kata huku akiongea na kuwasikiliza wananchi kero zao na kuwamwagia sera zake.
 |
| Wanafunzi wa Bonyokwa, wakiwa wamechoka kutokana na shule kuwa mbali, hapa wanapumzika. |
 |
| Mtatiro akiongea na kula wanachouza waasilia mali wadogo wa Bonyokwa |
 |
| Mtatiro na timu yake ya kampeni wakipanda milima kuwa kuuza sera zao kwa wannchi waliko, Bonyokwa |
 |
| Mtatiro na timu yake wakishuka mabonde kuwasikiliza wannchi na kumnadi mgombea urais wa UKAWA, LOWASSA |
 |
| Habagui mtu, hadi sehemu za kupumzika na kujipatia vinywaji yuko nao Wanabonyokwa |
 |
| Mtatiro akiwa na mgombea udiwani kata ya Bonyokwa Charles Kwiyeko(katikati) pamoja na aliyekuwa diwani wa viti maalumu wa CHADEMA Grace Shelukindo (kulia) |
0 comments :
Post a Comment