TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Chuo kikuu cha Dar es salaam kimepanga kuongeza mabweni ya wanafunzi ili kuhakikisha asilimia kubwa ya wanafunzi wanakaa katika mabweni ya chuo.
 
kauli hiyo ilitolewa jana na Depute Academic wa chuo hicho Prof Mgaya alipo kuwa akitoa ufafanuzi baada ya Makamu wa Raisi wa DARUSO kuelezea jinsi ilivyokuwa tatizo kwa upande wa hostel kwa wanafunzi.
 
akitoa ufafanuzi Mgaya alisema kuwa jana (jumamosi) mkuu wa chuo hicho alikuwa na kikao na kampuni lililojitokeza kujenga hosteli hizo na hivyo wanasubili makubaliano hayo ili kujua mpango wa ujenzi utaanza lini.
 
tatizo hilo limekuwa kubwa kwa chuo hicho kutokana na idadi ya wanafunzi wanao jiunga na masomo kuwa wengi kuliko idadi ya vyumba vya kulala vilivyopo.
 
mpaka sasa wanafunzi wa mwaka wa kwanza tu, ndio huwa wanpewa uhakika wa kupata vyumba na kwa wanafunzi wa mwaka wa pili, watatu na kuendelea ni wachache tu ndio wanaopata nafasi za vyumba. Wengi wao hupanga vyumba au hosteli za nje ambazo ni ghalama saana na hivyo kuwasababishia ugumu wa maisha wanafunzi hao.
 
kwa uapande wa wanafunzi wa SJMC-UDSM Prof Mgaya alisema kuwa wanatarajia ifikapo mwezi wa kumi, mhula wa masomo utakapo anza, wanafunzi waanze kukaa katika mabweni yaliyoko Kijito nyama Poster.
 
kujengwa kwa mabweni hayo itakuwa ni furaha kubwa kwa wanafunzi hao kwai kwao ni kilio cha mda mrefu.

0 comments :

 
Top