Kiongozi wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria
|
Kiongozi mmoja wa kanisa la kianglikana anayehusika katika
majadiliano ya kuwaachilia huru mamia ya wasichana waliotekwa nyara nchini
Nigeria amesema kuwa wengi wao wanazuiliwa nje ya taifa hilo katika kambi tatu
tofauti.
Daktari Steven Davis ambaye ni raia wa Australia ameiambia BBC kwamba wenzake
waliwaona baadhi ya wasichana hao ambao walikuwa wakioga na upande mwengine
kuwapikia waliowateka kutoka kwa kundi la wanamgmbo wa Boko Haram.
Davis amesema kuwa majadiliano ya kutaka kuwachiliwa kwa wasichana hao
karibia yafue dafu kabla ya baadhi ya makamanda wa kundi hilo kulipinga wazo
hilo dakika za mwisho wakihofia kukamatwa.
Amesema juhudi zozote za kuwanusuru wasichana hao kwa nguvu hazitafua
dafu.
Chanzo BBC Swahili
0 comments :
Post a Comment