TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749




Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania nafasi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2019. 

Bila ya kutoa sababu za kuchukua uamuzi huo, maafisa nchini Kongo wamesema hata ziara ya timu ya maafisa wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAN) iliyokuwa ifanyike mwezi huu imefutwa. 

Sasa nchi zilizobakia kwenye kinyang'anyiro hicho ni Algeria, Cameroon, Guinea, Cote d'Ivoire na Zambia, na nchi itayobahatika kuwa mwenyeji wa CAN 2019 itajuilikana mwezi Septemba. 

Mwakani Morocco ndiyo itakayoandaa mashindano hayo, ambapo Libya itakuwa mwenyeji wa michezo ya 2017.

0 comments :

 
Top