TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Moshi. Mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo amemtaka Rais Jakaya Kikwete na chama chake, CCM kuwa makini na msimamo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akisema haamini kama umoja huo umesema kila unachokusudia kukifanya.
Badala yake Kisumo alisema kinachofanywa na Ukawa ni mbinu za kujiimarisha kisiasa, jambo alilolisema iwapo CCM na Serikali yake haitakuwa makini, huenda ikaingia katika mtego na kushindwa kujinasua baada ya umoja huo kuimarika.
Kauli ya Mzee Kisumo imekuja wakati ambao viongozi wa Ukawa wameendelea kusisitiza kwamba wataendelea kususia vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoanza mjini Dodoma, Agosti 5 mwaka huu, hadi pale madai yao yatakapozingatiwa.
Ukawa ambao unaundwa na Vyama vya Chadema, NCCR Mageuzi, CUF na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais, wanasisitiza kwamba lazima Bunge hilo lijadili Rasimu ya Katiba kama ilivyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na wakitaka pendekezo la muungano wa serikali tatu lizingatiwe.
Kamati zote 12 za Bunge hilo katika maoni ya wengi zilipendekeza muundo wa Serikali mbili tofauti na uliopendekezwa katika rasimu ya Katiba iliyoandaliwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kisumo alisema kinachotakiwa ni Ukawa kurudi bungeni wakabishane kwa hoja na kama wakishindwa, bado wenye uamuzi wa mwisho juu ya Katiba ni wananchi kwa kupiga kura ya ndio au hapana.
Source Mwananchi

0 comments :

 
Top