TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


KWANINI SERIKALI YA DARUSO INADHIHAKI WANAFUNZI AMBAO.HAWAJAPATA FEDHA ZA FIELD???
Ndugu zangu wana UDSM sote tunafahamu mateso ambayo wanafunzi ambao bado hawajapata fedha za field wanavyoteseka, wanavyofedheheka na hata kudhalilika.. 
Seikali ya DARUSO imekaa kimya licha Rais Filbert Nickson kuwadanganya wana UDSM tena kwa maandishi wakati anaenda Korea kusini, kuwa watapata fedha zao wote katika wiki ya mwisho ya mitihani..
Baada ya Rais kukaa Korea kwa wiki mbili na kurudi nchini alikuta asilimia 88 na wanafunzi aliowaahidi fedha za field wakiwa bado hawajapata fedha zao, lakini cha AJABU NA KUSIKITISHA hakuweza kutoa neno lolote la ufafanuzi..

Wana UDSM tumekuwa tukipiga sana simu kwa waziri mkuu na Rais wa DARUSO kupata ufafanuzi wa suala hili lakini zimekuwa hazipokelewi na sms pia hazijibiwi..
Tunaambiwa kuwa wakuu wetu hawa wapo busy na PROGRAM YA UONGOZI INSTITUTE, program ambayo inawawezesha kupata posho ya sh. Elfu ishirini na nane kwa siku pamoja na chakula na malazi..

Wakati huo asilimia 88 ya wana UDSM wanaendelea kutaabika kwenye maeneo yao ya field bila kupata uhakika wa kuendelea na mchakato huo wa kitaaluma au lah. 
JANA TUKAPEWA TAARIFA MPYA, iliyosambazwa na waziri wa katiba na sheria HUKU IKIWA NA MUHURI WA DARUSO kuwa serikali ya DARUSO inawahakikishia wana UDSM kuwa wanafunzi wa college zote ambao hawajapata fedha za field kuwa watapokea fedha hizo siku ya jana.. tofauti na hapo UAMUZI MGUMU UTACHUKULIWA, 

Hapo ndipo wana udsm walipolipuka kwa furaha kila eneo walilopo, furaha ya kwanza ikiwa ni uhakika wa kupokea fedha na furaha ya pili ni SERIKALI YAO KUCHUKUA UAMUZI MGUMU kama ilivyoahidi tena kwa hiari ili kuweza kunusuru MAISHA na TAALUMA zao popote pale walipo.

lakini kwa kuwa njia ya MUONGO NI FUPI na MUNGU HUWA HAMFICHI MNAFIKI siku ya jana tarehe 22 july ikamalizika bila AHADI YA RAIS, WAZIRI MKUU na WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA kutimia, Kwa kuwa ahadi haikutimia wana UDSM wote wakasubiri kutangaziwa uamuzi mgumu utakaowaokoa kutoka kwenye TOPE WLILOPO, lakini wapi bhana, serikali chini ya WAZIRI MKUU, RAIS NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA PAMOJA NA WAPAMBE WENGINE waliamka asubuhi na mapema na kuamua kuvaa sare sare

Viongozi wa DARUSO wakiwa kwenye mapozi ya picha ya pamoja, asubuhi wakitoka Chuo kuelekea bodi ya mikopo

Na kisha kwenda makao makuu ya bodi na kuanza kupiga picha za dhihaka kuwa bado wanatafakari kufanya maamuzi magumu, lakini pia wakaenda mbali zaidi na kupiga picha zingine za mapozi wakiwa kwenye milango mbalimbali ya bodi ya mikopo, 


Viongozi wa DARUSO wakiwa na Waziri Mkuu (mwenye suti nyeusi katikati) wakiwa ofisi za bodi ya mikopo


Milango ambayo wenyeviti wa college na naibu waziri wa mikopo walishaingia sana wakitafuta majibu juu ya fedha za field na kuishia kupigwa ahadi tu,

Ndugu zangu hivi kulikuwa na haja gani kwa RAIS, WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA kuwadhihaki wana UDSM kuwa fedha zitatoka jana?  Na kulikuwa na sababu gani ya kuwahadaa watu  kisaikolojia kuwa UAMUZI MGUMU UTACHUKULIWA? 

Hivi ndugu zanguni wana UDSM uamuzi mgumu ni KUVAA SARE NA KWENDA BODI YA MIKOPO KUULIZA FEDHA ZITAINGIA LINI? 
Pengine kwa kuwa watu hawa walioenda bodi leo ilikuwa mara yao ya kwanza kuingia ndio maana ilibebeshwa jina La uamuzi mgumu, kiukweli hii ni fedheha kwasababu KWENDA BODI KWA MARA YA KWANZA NA KUINGIA NDANI HAIWEZI KUWA UAMUZI MGUMI HATA MARA MOJA.

Mbaya zaidi, kwa kuwa tangazo lililotolewa jana lilioneshwa kuwa uamuzi mgumu utachukuliwa mpaka sasa hv HATUJAONA TANGAZO LINGINE LIKISEMA UAMUZI MGUMU ULIOCHUKULIWA, sihamasishi MGOMO WALA MAANDAMANO ILA NAHOJI UAMUZI MGUMU TULIOAHIDIWA NA SERIKALI YETU YA DARUSO..

kiukweli Wana udsm TUMEDHIHAKIWA SANA NA UAMUZI MGUMU ULIOCHUKULIWA NA RAIS, WAZIRI MKUU PAMOJA NA WAZIRI WA SHERIA NA KATIBA, bila kuwashirikisha hata Vice president na naibu waziri wa mikopo aliyepo hapa chuo ILI VICE NA NAIBU WAZIRI WA MIKOPO nao waweze kutoa maoni yao juu ya UAMUZI MGUMU WA KUVAA SARE NA KUPIGA PICHA WAKIWA NA SURA ZA BASHASHA KATIKA MILANGO YA BODI wakiamini kufanya hivyo kutafanya waonekane wafuatiliaji wazuri na wenye uchungu na fedha za field..
KWELI AKUTUKANAYE HAKUCHAGULII TUSI..
shikamooni mlio vaa sare na kupiga picha za BASHASHA.


0 comments :

 
Top