TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo(Jumatano) asubuhi.
Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani. Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea.
Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kulifikisha wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.
Edwadi Lowasa akiwa kama mbunge amesema amejitolea msaada wa kuwasfirisha wanafunzi kurudi kwao hadi marekebisho yatakapo fanyika.
"Mimi Kama Mbunge wa Monduli nimetembelea shule hiyo na kuwahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida."

Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao inafikia kiasi cha shilingi laki Saba.
Aidha aliongeza kuwa yeye akiwa kama mbunge wa Monduli kwa kushirikiana na kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
POLENI SANA WOTE MLIOPATA AJALI HII YA MOTO MIMI KAMA MBUNGE WENU NIPO PAMOJA NA NYINYI. Huu ni ujumbe kutoka kwa Lowasa...

0 comments :

 
Top