TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


                                                  Leo mida ya saa tisa, ilikuwa arobaini kwa tapeli, kibaka na mchomoaji maarufu maeneo ya Poster karibu na Benki ya NBC. Mtu huyo mwenye umli wa miaka 40 ambaye jina lake halikufahamika, alikamatwa na makachero wa polisi ambao walidai walikuwa wakimfuatilia kwa mda mrefu kwani mchezo wake huwa ni kuwafuatilia kwa nyuma watu waliotoka kuchukua pesa Benki, wazungu, na mtu yeyote mwenye begi mgongoni au mkononi. Na mbinu yake kubwa ni kuchana begi na kuondoka na anachokikuta.         
Wakieleza makachelo hao, walisema kuwa pia jamaa huyo anakesi nyingi za namna hiyo kituo cha polisi Poster.
Akiulizwa juu ya makovu aliyo nayo kichwani mwake kama hayatokani na kupigwa na watu wanaomkamata akiwaibia, mwizi huyo alikubali nakusema ni takribani mara nyingi sanaa hupingwa na kuzimia.

Polisi walionekana kuchoshwa na tabia ya huyo jamaa kisi cha kumuambia kuwa wangekuwa maeneo ya Tandika, wangemwachia ashughulikiwa na wananchi anaowaliza kila siku.

0 comments :

 
Top