
Nchini Marekani, baraza la wawakilishi ambalo linadhibitiwa na chama cha Republican limepiga kura kuwasilisha mahakamani kesi dhidi ya rais Barack Obama. Hatua hiyo inawaruhusu wanasheria wa bunge hilo kuandika waraka wa sheria unaotarajiwa kudai kuwa Obama alikiuka mamlaka yake wakati alipofanya mabadiliko katika sheria ya matumizi ya afya, yanayofahamika kama "Obamacare". Obama anadai kuwa alitumia madaraka yake kama hatua ya mwisho baada ya bunge la Marekani kukataa kushirikiana naye kufanya kazi.Je, ni sawa Rais wa nchi kushtakiwa kutokana na maamuzi aliyoyafanya kwa manufaa ya umma?
Source DW
0 comments :
Post a Comment