TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Wanafunzi wasiopungua 513 wa shule za sekondari za Nkuyu, Kyela, Keifo,Itunge, Mwaya na Ikolo zote za Wilayani Kyela mkoa wa Mbeya, walipelekwa kituo cha polisi cha Kyela, na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kyela Gabriel Kipija akisaidiana na mkuu wa wilaya kwa sababu ya kuchelewa kwenda shuleni.

Inasemekana chanzo cha kukamatwa kwa wanafunzi hao, inatokana na matokeo mabaya waliyopata katika mtihani wa kidato cha nne kwani Wilaya ya kyela imekuwa ya mwisho kati ya halmashuri za Wilay kumi za Mkoa wa Mbeya.

Matokeo hayo yalisababisha hasira kwa viongozi mbalimbali wa wilaya ya Kyela, hasa Mwenyekiti wa halmashauri pamoja na mkuu wa wilaya.

Walipo waona wanafunzi wanachelewa wakaamua kuwapeleka polisi ili wawaonyeshe ni jinsi gani wanakerwa na kitendo cha wanafunzi kufeli mitihani na huku chanzo kikiwa ni uzembe wa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na uchelewaji wa wanafunzi kuingia darasani hivyo kukosa baadhi ya masomo yanayofundishwa asubuhu

Wanafunzi waliachiwa siku hiyohiyo baada ya wazazi wao kufika kituo cha polisi, huku baadhi ya wazazi wakiwa na jaziba ya watoto wao kupelekwa polisi.


0 comments :

 
Top