TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

Mume wa mwanamuziki wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameapa kwa kulamba kidole, kukichovya kwenye mchanga kisha kukipitisha shingoni kuwa, hana mpango wa kurudiana na mkewe huyo katika maisha yake. Mbasha alikiri kufanya jitihada za ziada akiwatumia ndugu, jamaa na marafiki kumshawishi Flora kurejesha upya penzi lao, lakini amekuwa akiambulia maneno makali na matusi.
“Mimi na Flora basi tena, acha ibaki historia, amenitesa sana kihisia,” alisema Mbasha.
source: GPL

0 comments :

 
Top