TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749


Redio ya kijamii Kyela FM, iliyoko Kyela mkoani Mbeya, imefungiwa na TCRA kurujsha matangazo yake kuanzi tarehe 03 August 2015 kutokana na kile kilichoitwa utovu wa nidhamu na kiburi kilichoonyeshwa na wamiliki wa redio hiyo.
Kutoka chanzo kimoja cha habari hiyo kilisema kuwa Aidha TCRA wamechukizwa sana na kitendo cha wamiliki kuanza kumwaga chuki kwenye mitandao ilihali walikataa barua.
Wakati huohuo, kitendo hiki kimetafsiriwa kitofauti na watu mbalimbali, huku wengi wakisema kuwa ni chuki za kisiasa dhidi ya mmiliki wa redio hiyo ambaye alikuwa ni mtangaza nia ya ubunge kupitia CCM akichuana na Mwakyembe ambaye aliibuka mshindi.
Akitoa malalamiko yake mmiliki wa Mkurugenzi wa redio hiyo George Mwakalinga, kupitia facebook alionesha kumtupia mpira aliyekuwa mbunge wa Kyela, Mwakyembe kwa kile alichokiit ni upotoshaji kwa jamii kuhusu sakata hilo.
Alieleza kuwa Mwakyembe ameongea kupitia CHAI FM kuhusu suala la kufungiwa kituo cha redio cha Kyela fm.
"Kwa mara nyingine ameendelea kudanganya na kupotosha wananchi kwa kudai kwamba Kyela fm wamepewa onyo mara nyingi na tcra. Ukweli ni kwamba kyela fm hawajawahi kupewa onyo hata mara moja. Kyela fm inakanusha vikali uongo huo na kama ana ushahidi wowote basi auweke wazi.

Pia, ametoa sababu za kufungiwa kituo kwamba ni watangazaji kuegemea upande wa mkurugenzi wao kwenye kampeni za uchaguzi. Kwahiyo anathibitisha sababu ya kufungiwa ni kutokana na vipindi vya siasa za kura ya maoni ndani ya ccm. Hili ni tofauti na hoja mpya ya TCRA kwamba sababu ni transmitter au sababu ni leseni.
Tunamwomba mheshimiwa Mwakyembe awe mkweli na awaambie wananchi, simu aliyopiga kwa uongozi wa tcra tarehe 24/07 ilikuwa kuhusu nini? Pia tunamwomba kama waziri mwandamizi katika serikali, awaombe TCRA waweke wazi sababu za kufungiwa kituo.
Ni ukweli tu unadumu. Siasa za uongo, ubabe na visasi haziwezi kuisaidia Kyela. Wakati wa kampeni aliongea uongo pia kwa kusema kwamba Kyela fm ililetwa iwe redio ya halmashauri lakini Mwakalinga akaiporana kuifanya yake. Ulikuwa uongo usio hata na chembe ya ukweli." aliandika Mwakalinga
Kwa upande wake meneja wa redio hiyo Maisha Ambangile aliueleza uma kupitia facebook kuwa ufungaji wa redio huo ulifanywa na watu ambao hakupata nafasi ya kukariri majina yao walipokuwa wakimtajia kujtokana na tahamaki kubwa aliyokuwa nayo isipokuwa alifanikiwa kushika vyeo tu.
Alieleza kuwa watu waliowasili kuifunga redio hiyo walijitambulisha kwa vyeo vya,  Mkuu wa kitengo cha matangazo kutoka makao makuu (TCRA-Dar), Mwanasheria Mwandamizi (TCRA-Dar), Meneja Wa Kanda ya juu kusini -Mbeya (Lilian Mwangoka), Inspector Wa polisi kutoka ofisi ya RPC-Mbeya, Na mkuu wa upepelezi Wilaya ya Kyela.
Lakini alieleza kuwa baada ya utambulisho huo alipewa barua aisaini lakini alikataa kufanya hivyo kutokna na makosa ya barua hiyo.
"Baada ya utambulisho huo, mkuu wa kitengo alimwamuru Mwanasheria kunipa barua na kusaini na kukubali nimeipokea....na barua hiyo ikielekeza (Addressed) kwa Mkurugenzi wa Radio, Mimi (Meneja) nikagoma kusaini kwasababu kwanza barua haijaeleza sababu ya kufunga Radio, pili Mimi sio Mkurugenzi wa Radio. Kwahiyo ikagoma Kusaini wakati majibizano yakiendelea wakaamuru niwapeleke kwenye studio na Kuzima Radio na kutoruhusiwa Kuwaiwasha kwa muda usiojulikana." Alieleza Ambangile
Hata hivyo meneja wa redio hiyo alieleza kuwa uongozi wa redio hiyo unaraani hujuma inazofanyika juu yao, lakini pia kuwanyima haki ya kimsingi wananchi ya kusikiliza na kuabarishwa katika matukio mbalimbali yanayojiri ndani na nje ya Kyela.

0 comments :

 
Top