TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

katika kipindi hiki cha kampeni na kabla ya kampeni CCM imefanya mipango yake kwa kukurupuka, zisizo na ubunifu wa kisomi na kutotambua ni nini wanakitaka kwa wananchi ili washinde uchaguzi wa mwaka huu.
CCM imetumia maneno ya kuchefua wananchi na kuonyesha wazi kuwa imejiandaa kufanya fitina za kila namna ili mgombea wao ashinde. Kitendo hikikilikuwa ni kosa la kwanza, kwani ilisaidia vyama vingine kuanza kujipanga zaidi na wananchi waanze kujipanga kufanya namna ya kurinda kura.
Kwa chama ambacho propaganda zake ziko vizuri ingeyaweka sawa mambo kama kauli za viongozi kutoka CCM walizokuwa wakizitoa kama vile, gori la mkono, mwali ninaye mimi, wapumbavu na marofa, tutashinda kwa namna yoyote ile.
Kosa la pili ni kufanya baadhi ya mambo mapema kiasi kwamba inatoa nafasi kwa wapinzani kuulemisha umma kuhusu mambo hayo na wannchi kuanza mapema kutengeneza hasira na jinsi ya kuwaadhibu na kuwadhibiti CCM. Kwa mfano: kitendo cha kuanza mapema kukataza wananchi ubaki kusubiria matokeo mita 200 kama seria inavyosema. Hii imesiadia vyama vya upinzani kuenda mahamani na kuwaonyesha wannchi jinsi CCM walivyo na hira.
Kitu pekee ingekifanya ni kutoa matamko kama haya siku moja kabla ya siku ya kupiga kura, hii isingetoa mwanya kwa wnanchi kupata ufafanuzi wa suala hilo kutoka kwa wanasiasa. Wananchi wasingekuwa na ujasiri wa kufanya lolote siku ya kesho yake kwani wangebaki na sintofahamu.
Jambo la tatau ni kuwaandikisha wannchi mwaka huu wakiwa tayari na mwamko mkubwa hasa kwenye mikoa mikubwa ambayo iliandikishwa baada ya viongozi kutangaza nia na wengine kukatwa kwa hira.
Ikasababisha hadi wasikuwa na nia ya kujiandikisha kufany ahivyo kwani tayari walishakuwa na mwamko kutoka kwa wanasiasa. 
Jambo la mwisho watakalo lifanya ni kutumia nguvu ya vyombo vya ulinzi kukataza wannchi kufanya baadhi ya vitu ambavyo wamezoea kuvifanya kila siku na hata kipindi cha uchaguzi. Kwa mfano, kitendo cha kukataza mikesha, baa kufungwa wakati zinakibari cha kufanya shughuli zake kwa kukesha. Hii inaibua hasira kwa wananchi na kusaidia kesho yake kwenda kuwapigia upinzani kwani wao sio wenye serikali inayotoa maagizo.
Hivyo CCM, mnajiua wenyewe kwa mipango yenu, mgejua kuwa mtashinda kwa gori la mkono, mngekuwa fair kwa kipindi hiki ili wanasiasa ndio wawe wanalalamika tu pasipokuwa na ushahidi wa kauli, vitendo au hata viashiria. mungewapumbaza wannchi kutoamini maneno ya wansiasa na wangeamini ni kampeni tu, huku nyi mkifanya mikakati chini kwa chini juu ya gori la mkono.
MMEJIUA WENYEWE NA MSILAUMIANE, HAYA NI MADHARA YA KUFANY AKAZI KINDUGU, MNATAFUTA WATAALAMU WENU AMBAO WALIPEWA KAZI SIO KWA UBUNIFU WAO AU UTENDAJI WAO, ILA NI KWASABABU YA MFUMO.

0 comments :

 
Top