1.
Kama mnavyofahamu, JWTZ linashiriki katika operesheni za Umoja wa
Mataifa huko Goma DRC. Kikosi chetu kimeendelea kutekeleza majukumu yake
ya kulinda amani kama kinavyopangiwa na Jeshi la Umoja wa Mataifa
nchini DRC lijulikanalo kama MONUSCO.
2. Tarehe 28 Agosti 2013
wanajeshi wetu wakiwa katika eneo lao la Ulinzi waliangukiwa na bomu
katika eneo hilo na kusababisha majeruhi. Wakati wanapelekwa hospitali
kwa matibabu, kwa bahati mbaya mwanajeshi wetu mmoja, Meja Khatibu
Mshindo alifariki dunia. Majeruhi wengine wanaendelea na matibabu, na
hali zao zinaendelea vizuri.
3. MONUSCO inaandaa utaratibu wa kuleta mwili wa marehemu.
Imetolewa na: Kurugenzi ya Habari na Uhusiano Makao Makuu ya Jeshi. Dar es Salaam.
0 comments :
Post a Comment