TUMA HABARI YOYOTE ULIYONAYO KWENDA zimetokelezea@gmail.com AU Whatsapp No 0716790749

January Makamba na Benard Membe wamepatikana na hatia ya kosa la kufanya kampeni kabla ya muda kinyume cha taratibu na kanuni za CCM.
Ngeleja na Lowassa wamekutwa na makosa matatu kila mmoja ambayo ni uadilifu, kutoa rushwa na kufanya kampeni kabla ya muda.

Lowassa ameonekana kuwa na utovu mkubwa wa nidhamu kwani amedaiwa kusambaza fomu za udhamini kabla ya muda huku akihonga watu kuchukua kadi mpya za chama maeneo ya Zanzibar kinyume cha sheria.

Pia Lowassa na Membe wamedaiwa kukigawa vibaya chama pamoja na vyombo vya habari hali iliyotafsiriwa kuwa ni makosa kulingana na miiko ya CCM.

Kwa maana hiyo mashitaka yote yanapelekwa kamati kuu ya CCM kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

Leo usiku hatima ya hawa wote itajulikana. Sisi tutakuwepo kumulika kwa macho kama paka
 

KUPITIA VYOMBO VYA HABARI MAGAZETI YA LEO TAARIFA KAMA HIZI ZIFUATAZO ZITAWAPA YANAYOENDELEA DOM.
1: Uhuru
Front Page ''Waliokiuka Kanuni ''out''.-Hiki ni chombo kikubwa sana cha CCM

2:Rai
''Lowasa afitiniwa''

3: Shuhuda
''Kikwete Atajwa ''KUMMALIZA'' Lowasa.

4: Umma Tanzania
''Kiwewe Kambi Ya Lowasa''

0 comments :

 
Top